Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amemwapisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Jacob Mkunda huku akiahidi kumpangia majukumu mengine CDF aliyemaliza muda wake, Jenerali Venance Mabeyo. Hafla ya la kumwapisha Jenerali Mkunda ilifanyika leo Alhamisi Juni 30, 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam. Mkuu huyo wa nchi pia amemwapisha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi…