
Viongozi wa kidini wakutana mashariki mwa Kongo kujadili hali ya mambo
Viongozi wa kidini wamekutana katika mji wa Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kufuatia machafuko yaliyosababisha vifo vya watu 50 mashariki mwa nchi hiyo. Itakumbukwa kuwa, Alhamisi iliyopita jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lililituhumu kundi la waasi la M23 kwa mauaji hayo na kukiuka mapatano ya kusitisha vita yaliyofikiwa hivi karibuni. Mchungaji Samuel…

Rwanda yaafiki ‘kusitishwa mapigano mara moja’ mashariki mwa DR Kongo
Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta na Rais Paul Kagame wa Rwanda wamekubaliana juu ya haja ya waasi wa M23 kusitisha mapigano na kuondoka katika maeneo waliyoyateka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Hayoa yameelezwa kwenye taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Taarifa hiyo ya EAC imeongeza kuwa: Kenyatta na Kagame…

EAC yasisitiza kupatiwa ufumbuzi mgogoro wa Kongo
Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamekubaliana katika kikao kilichofanyika Cairo, Misri kwamba mgogoro wa mashariki mwa Kongo unapasa kutatuliwa kwa njia za kiraia na kupitia mazungumzo. Maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yameathiriwa na ukosefu wa amani tangu miaka 20 iliyopita ambapo mapigano kati ya vikosi vya serikali na makundi…

Wakongo wafanya mandamano makubwa dhidi ya waasi wa M23 mjini Bukavu
Wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wenye hasira wamechoma moto bendera ya Umoja wa Ulaya katika mji wa Bukavu mashariki mwa nchi hiyo, huku mamia ya wakiandamana dhidi ya waasi wa M23. Wananchi hao wameeleza kutoridhishwa kwao na uingiliaji wa mataifa makubwa kama vile Marekani, Uingereza na Ufaransa katika masuala ya ndani ya nchi…

DRC na Rwanda zakubaliana kupunguza mivutano kwa sababu ya waasi wa M23
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC na Rwanda zimekubaliana kutekeleza “mchakato wa kupunguza mvutano” baina yao kufuatia mazungumzo ya siku moja yaliyofanywa na marais wa nchi hizo mbili kwa upatanishi wa rais wa Angola. Hayo yameelezwa na ofisi ya rais Felix Tshisekedi wa DRC, katika ujumbe uliotumwa kwenye mtandao wa Twitter. Aidha, Jamhuri ya Kidemokrasia…

WHO: Mripuko wa nne wa Ebola katika jimbo la Equateur, DRC umetokomezwa
Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza kuwa, mripuko wa Ebola uliotangazwa tarehe 23 mwezi Aprili mwaka huu huko Mbandaka, mji mkuu wa jimbo la Equateur katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umetokomezwa. Taarifa iliyotolewa na WHO katika miji ya Kinshasa, DRC na Brazzaville, Jamhuri ya Kongo, imesema mripuko huo ulikuwa ni wa 3 kwa jimbo la…

Mjumbe wa UN Kongo alitahadharisha Baraza la Usalama kuhusu hali ya usalama Kongo
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Bintou Keita amelitahadharisha Baraza la Usalama la umoja huo kuhusu machafuko ambayo yanaweza kuibuka mashariki mwa nchi hiyo ambako makundi ya wanamgambo wenye silaha yanaongezeka kila siku. Akizungumza katika mkutano wa Baraza la Usalama la UN, Bintou Keita amesema kuwa, iwapo kundi la waasi wa…