Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo inatarajia kuwafanyia upasuaji wa kuwatenganisha pacha walioungana kifuani. Upasuaji huo unakadiriwa kutumia saa saba na utafanywa na wataalamu wa afya 31 kutoka Tanzania na Ireland ambao wanatokea Shirika la Operation Child Life. Tanzania itakuwa nchi ya tatu baada ya Misri na Afrika Kusini katika bara la Afrika…