
Poland: Nishati ya amani ya nyuklia ni haki ya kimsingi ya mataifa yote duniani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland ameyalaumu madola yaliyohodhi nguvu za nyuklia duniani na kusema kuwa, inabidi mataifa ya dunia yashirikiane pamoja kufaidika kwa njia za amani na nguvu za atomiki na kusitumiwe vikwazo kama njia ya kuyazuia baadhi ya mataifa kufaidika na haki yao hiyo. Marekani iko mstari wa mbele kuziwekea vikwazo nchi…

Onyo la Katibu Mkuu wa UN la kutokea vita vya nyuklia duniani
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonya kuhusu hatari ya kutokea vita vya nyuklia duniani. Alitoa onyo hilo Jumatatu, Agosti 1, 2022 wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kuangaliwa Upya Mkataba wa NPT wa Kuzuia Uzalishaji na Uenezaji wa Silaha za Nyuklia. Katika mkutano huo uliofanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New…

Mauaji ya Ayman al Zawahiri yapokewa kwa hisia tofauti
Mauaji ya Ayman al Zawahiri, kiongozi wa mtandao wa al Qaida katika operesheni ya droni iliyofanywa na wanajeshi wa Marekani, yamepokewa kwa hisia tofauti ya duru za kisiasa za nchi hiyo. Mapema leo asubuhi, rais wa Marekani, Joe Biden ametangaza habari ya kuuawa Ayman al Zawahiri katika shambulio la ndege isiyo na rubani lililofanywa na…

Iran inaunga mkono kikamilifu sera ya ‘China Moja’, inapinga ‘uharibifu’ wa Marekani
Rais wa Iran Ebrahim Raisi anasema kuheshimiwa mamlaka ya kitaifa na kulindwa mipaka ya ardhi ya nchi ni miongoni mwa kanuni za kimsingi za sera za kigeni za Tehran huku akitangaza uungaji mkono thabiti wa Jamhuri ya Kiislamu kwa sera ya China Moja kuhusiana na Taiwan. “Uungaji mkono kwa sera ya China Moja ni sera…

Magendo ya binadamu yameongezeka mara 26 katika mpaka hatari zaidi duniani
Wizara ya usalama wa ndani ya Marekani imetangaza kuwa, pato linalopatikana katika biashara haramu ya magendo ya binadamu inayofanywa kupitia mpaka wa pamoja wa nchi hiyo na Mexico, ambao ni mpaka hatari zaidi duniani, limeongezeka kutoka dola milioni 500 mwaka 2018 na kufikia dola bilioni 13 kwa sasa. Tovuti ya gazeti la New York Times…

Ubaguzi wa rangi dhidi ya watu wenye asili ya Asia umekithiri Marekani
Matokeo ya utafiti uliofanywa katika majimbo mbalimbali ya Marekani yanaonyesha kuwa, vitendo na mienendo ya ubaguzi wa rangi dhidi ya raia wa nchi hiyo wenye asili ya Asia imeongezeka katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Kwa mujibu wa gazeti la The Guardian, matokeo ya utafiti uliofanywa katika majimbo tofauti ya Marekani na kituo cha binafsi…

Jen. Shekarchi: Marekani, Israel zinajua vyema gharama ya kuitishia Iran
Msemaji wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran amesema Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel zinatambua vizuri kile ambacho kitawafika iwapo zitathubutu kutelekeza kivitendo vitisho vyao dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. Brigedia Jenerali Abolfazl Shekarchi, Msemaji wa Jeshi la Iran amesema ukongwe wa Rais Joe Biden na tabia yake ya kupenda kulala ndiyo imempelekea atumie lugha…

Marekani yatangaza vikwazo vipya dhidi ya sekta ya mafuta ya Iran
Wizara ya Fedha ya Marekani imeendeleza uraibu wa nchi hiyo wa kuziwekea vikwazo nchi mbalimbali kwa kutangaza vikwazo vipya dhidi ya sekta ya mafuta na petrokemikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Wizara ya Hazina ya Marekani jana Jumatano ilitangaza kuziwekea vikwazo kampuni mbalimbali zenye makao yao katika Umoja wa Falme za Kiarabu, eti kwa kufanikisha…