Waislamu Marekani wataka uchunguzi baada ya Msikiti kuhujumiwa California
Mhalifu anayeaminika kuwa mwenye chuki dhidi ya Uislamu amehujumu Kituo cha Kiislamu cha Tracy na Msikiti wa Tracy katika jimbo la California la Marekani mkesha wa mwaka mpya. Tukio hilo lilinaswa kwenye video ya usalama ambayo inaonyesha mshukiwa akirusha jiwe kubwa kupitia dirisha moja la msikiti huo. Basim Elkarra, mkurugenzi mtendaji wa Ofisi ya Sacramento…
Kuendelea mwenendo wa kufutwa kazi wafanyakazi huko Marekani; Amazon kupunguza wafanyakazi elfu 18
Mkurugenzi Mtendaji wa Amazon amesema kuwa kampuni hiyo itawafuta kazi wafanyakazi zaidi ya 18,000. Baadhi ya waajiri wakubwa wa Marekani, ikiwa ni pamoja na Walmart, Facebook na Pepsi, hivi karibuni wamepunguza maelfu ya nafasi za kazi nchini humo. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Andy Jaycee amesema leo Alhamisi kwamba idara muhimu zitakazopunguziwa…
Asilimia 70 ya Wamarekani wana wasiwasi wa kutokea vita vya nyuklia
Uchunguzi wa hivi karibuni wa maoni unaonesha kuwa asilimia 70 ya wananchi wa Marekani wana wasiwasi wa kutokea vita vya nyuklia. Kuendelea vita nchini Ukraine na vikwazo dhidi ya Moscow sambamba na kuendelea nchi za Magharibi kuirundikia silaha Ukraine ni sababu ya wasiwasi huo wa asilimia kubwa ya Wamarekani kuhusu kutokea vita vya atomiki duniani….
Bunge la Marekani lashindwa kumpata Spika; McCarthy ang’ang’ania licha ya kuangushwa mara tatu
Baraza la Wawakilishi nchini Marekani jana lilishindwa kumpata Spika mpya wa Bunge la nchi hiyo licha ya uchaguzi huo kufanyika mara tatu. Baada ya duru tatu za upigaji kura, Bunge liliahirisha mchakato huo hadi saa sita mchana leo Jumatano. Ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 100 ambapo hakuna Mrepublikan au Mdemokrat aliyeshinda uspika…
Wananchi Marekani hawamtaki Biden wala Trump kugombea tena katika uchaguzi 2024
Matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa hivi karibuni huko Marekani yanaonyesha kuwa akthari ya wapiga kura wa nchi hiyo wanapinga Joe Biden na Donald Trump, rais wa sasa na wa kabla yake, kugombea tena katika uchaguzi wa rais mwaka 2024. Uchaguzi ujao wa rais wa Marekani umepangwa kufanyika tarehe 5 Novemba mwaka 2024. Shirika…
Makumi ya Wamarekani, wahanga wa umaskini na baridi kali, huku mabilioni ya dola yakitumiwa kwenye vita vya Ukraine
Wakati mji wa Buffalo ulioko katika jimbo la New York kaskazini-mashariki mwa Marekani, ukihangaika kujikwamua kwenye athari mbaya za theluji na dhoruba kali, matatizo yaliyosababishwa na maafa hayo makubwa yamedhihirisha zaidi ukosefu wa usawa wa kiuchumi na ubaguzi wa kimbari katika mji huo na Marekani kwa ujumla. Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa, kukata tamaa…
Ripoti ya kutisha ya hali ya ukame duniani mwaka 2022
Ripoti zilizochapishwa kuhusu hali ya ukame duniani mwaka 2022 zinaonesha kuwa hali ya kutisha kuhusu ukosefu wa maji na mazao ya kilimo itaendelea katika miaka ijayo. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Iran (IRNA), ripoti na takwimu za kimataifa zinaonesha kuwa, mwaka 2022 ulitajwa kuwa mwaka wa ukame zaidi duniani katika miongo michache iliyopita, wakati…
Ufukara ndio uliosababisha vifo vingi vya baridi kali katika mji wa Buffalo, Marekani
Gazeti moja la Marekani limeandika kuwa, matatizo yaliyosababishwa na janga la kimbunga hatari na unyeshaji mkubwa wa theluji katika mji wa Buffalo yamedhihirisha zaidi ufukara na ukosefu wa usawa wa kiuchumi na wa mbari unaotawala katika mji huo wa Marekani kuliko ulivyowahi kushuhudiwa wakati mwingine wowote. Mji wa Buffalo ulioko katika jimbo la New York,…