
Marekani yatambuliwa kuwa mvunjaji mkubwa zaidi wa haki za wanawake
Afisa wa zamani wa vita vya kisaikolojia katika Jeshi la Marekani ametangaza kuwa serikali ya nchi hiyo ni mkandamizaji mkubwa zaidi wa wanawake duniani. Scott Bennett, afisa wa zamani wa vita vya kisaikolojia katika Jeshi la Marekani, amesema katika mazungumzo yake na Press TV kwamba Umoja wa Mataifa unapaswa kuangalia Marekani iwapo kweli unataka kugundua…

Waziri wa Usalama Marekani aeleza wasiwasi wake juu ya vurugu na machafuko ya ndani
Waziri wa Usalama wa Nchi wa Marekani ameeleza wasiwasi wake kuhusiana na ukatili na machafuko ya ndani akivitaja kuwa ni moja ya vitisho vikubwa vinavyofungamana na ugaidi wa ndani ya nchi hiyo. Matokeo ya uchunguzi wa mashirika ya kisheria na taasisi za utekelezaji wa sheria yaliyotolewa katikati ya mwaka huu wa 2022 yanaonyesha kuwa uhalifu wa…

Kukiri Marekani na Israel kuhusu kutotetereshwa Iran na machafuko ya hivi karibuni
Sambamba na himaya na uungaji mkono wa Marekani kwa wafanya fujo na machafuko nchini Iran, wachambuzi waandamizi wa masuala ya usalama wa Marekani na utawala haramu wa Israel wamekiri kwamba, Iran haijatetereshwa na machafuko hayo ya hivi karibuni. Avril Haines, Mkurugenzi wa Ujasusi wa Kitaifa wa Marekani sanjari na kuashiria vurugu na machafuko ya Iran…

National Interest: Vita vya pili vya ndani vimeanza nchini Marekani
Tovuti ya jarida la Marekani la National Interest limegusia vitendo vya kikatili vilivyofanywa na magaidi wa ndani ya Marekani na kusema kuwa, vita vya pili vya ndani vimeanza katika nchi hiyo ya Magharibi. Katika ripoti yake ya jana (Jumapili), shirika la habari la IRNA limelinukuu jarida hilo la Marekani likisema kuwa, watu waliofanya machafuko walikabiliana…

Kusambaratika siasa za vikwazo; Marekani yapigia magoti mafuta ya Venezuela
Baada ya kupita takriban miaka 10 ya vikwazo vikali vya Marekani dhidi ya Venezuela, hatimaye Washington imesalimu amri na imeamua kupigia magoti mafuta ya Venezuela. Marekani na waitifaki wake wakiwemo pia vibaraka wa ndani ya Venezuela, waliweka mashinikizo ya juu kabisa dhidi ya serikali ya Caracas kwa shabaha ya kuipindua serikali hiyo na kupandikiza mfumo…

Gazeti la Uhispania: Mechi ya Iran na Marekani ni mpambano mkubwa wa kisiasa
Gazeti la Marca la Uhispania limeitaja mechi ya soka ya michuano ya Kombe la Dunia kati ya timu ya taifa ya kandanda ya Iran na Marekani kuwa ni mpambano mkubwa wa kisiasa. Timu ya taifa ya kandanda ya Iran itamenyana na timu ya taifa ya Marekani katika mechi ya tatu ya hatua ya makundi ya…

Mbunge wa EU: Kwa nini Ulaya haikutaka Marekani iwekewe vikwazo ilipowaua Wairaqi kwa halaiki?
Mick Wallace, Mbunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya amesema, umoja huo ulionyesha undumlakuwili kwa kunyamaza kimya wakati askari wa jeshi la Marekani walipowaua kwa umati raia wa Iraq. Wallace, ameandika ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter wakati alipochangia ujumbe wa twitter uliozungumzia uhalifu na jinai zilizofanywa na jeshi la Marekani dhidi ya raia nchini Iraq na akasema: “kwa…

Amnesty International yaikosoa Marekani kwa kumpa kinga muuaji Bin Salman
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeukosoa utawala wa Rais wa Marekani, Joe Biden, baada ya Ikulu ya White House kutangaza kwamba mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman “ana kinga” inayozuia kushtakiwa katika kesi zinazohusiana na mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi. Shirika hilo pia limeikosoa Riyadh kwa…