
Wanajeshi 176 wa Marekani walijiua mwaka 2021
Idadi ya askari wanaojiua katika Jeshi la Marekani imezidi kuongezeka mwaka uliopita wa 2021 ambapo takwimu zinaonyesha kuwa askari 176 walijiua. Takwimu hizo za Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon, zinaonyesha kuwa, jeshi hilo limekuwa likijaribu kutafuta njia za kuimarisha kiwango cha maisha ya askari ili kuboresha afya yao ya kiakili. Tovuti ya military.com pia…

Maelfu waandamana nchini Ethiopia kupinga uingiliaji wa Marekani nchini humo
Maelfu ya Waethiopia walifanya maandamano ya nchi nzima siku ya Jumamosi kulaani kile walichokitaja kama uingiliaji wa madola ya kigeni, hasa Marekani, katika masuala ya ndani ya nchi yao. Katika mji mkuu Addis Ababa, waandamanaji walibeba mabango yaliyosomeka “Tishio kwa Ethiopia ni tishio kwa ulimwengu” na “heshimu uhuru wa kujitawala Ethiopia.” Mabango mengine yalikuwa na…

Mbunge wa Bunge la Ulaya: Marekani na Israel zinaunga mkono ugaidi
Mick Wallace, Mwakilishi wa Ireland katika Bunge la Ulaya amekosoa vikali sera za Marekani na utawala ghasibu wa Israel na kuzitaja kuwa waungaji mkono wa ugaidi. Mbunge huyo wa Bunge la Ulaya amelaani mauaji ya kizazi ya Saudi Arabia na Imarati huko nchini Yemen na kutangaza kuwa, Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel zinaunga…

Aghalabu ya Wademocrat wanatilia shaka iwapo Biden atagombea urais 2024
Akthari ya wafuasi na wanachama wa chama cha Democrat nchini Marekani wametilia shaka uwezekano wa Rais Joe Biden wa nchi hiyo wa kugombea muhula wa pili katika uchaguzi ujao wa rais wa mwaka 2024. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na USA Today ikishirikiana na Ipsos unaonesha kuwa, asilimia 56 ya wapigakura wa chama cha Democratic hawaungi…

Kitabu kipya chafichua hofu ya Trump ya kulipiziwa kisasi na Iran kwa mauaji ya Kamanda Soleimani
Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, aliwaambia rafiki zake kabla ya kumalizika muhula wake wa urais kuwa, alikuwa akihofia kwamba Iran ingejaribu kumuuwa ili kulipiza kisasi mauaji ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa mapinduuzi ya Kiislamu (Sepah). Hayo ni kwa mujibu wa kitabu kipya….

Kamanda wa Majeshi ya Iran aonya jeshi la kigaidi la Marekani na Israel
Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Meja Jenerali Mohammad Baqeri ametoa onyo kali na kusema ushirikiano wa jeshi la kigaidi la Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel pamoja na waitifaki wao waliowapa vituo vya kijeshi ni tishio kwa usalama wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Katika ujumbe, Meja Jenerali…

Russia yasisitiza kuhamishwa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kutoka New York
Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesisitiza kuwa Moscow inazingatia kikamilifu pendekezo la kuhamisha makao makuu ya Umoja wa Mataifa kutoka Marekani hadi sehemu nyingine. Alexey Drobinin, Mkurugenzi wa Idara ya Mipango ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema: “Katika miaka ya mwanzo mwa kuasisiwa Umoja wa Mataifa, wakati pande zote zilikubali kwamba makao…

Iran: Matukio ya karibuni ya Ukraine ni matunda ya uingiliaji wa Marekani
Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema kuwa, Marekani na nchi za Magharibi zinataka kutekeleza siasa zao za kibeberu katika maeneo yote hassasi na ya kiistratijia duniani na kwamba matukio ya Ukraine ni matunda ya mtazamo huo wa kiistikbari wa Magharibi. Shirika la habari la FARS limemnukuu Brigedia Jenerali Mohammad-Reza Gharaei Ashtiani akisema hayo jana wakati alipoonana na…