
Sonko aruhusiwa Kuwania Ugavana wa Mombasa, Presha kwa Abdulswamad Shariff Nassir
FARAAN:Majaji watatu wa Mahakama Kuu mnamo siku ya Jumatano tarehe 13 July 2022 walimruhusu aliyekuwa Gavana wa Nairobi, Mike Sonko kuwania wadhifa huo Mombasa, hatua inayotarajiwa kumtia presha mwaniaji wa ODM Abdulswamad Shariff Nassir. Bw. Nassir amekuwa kifua mbele kwenye azma ya kumrithi Gavana Ali Hassan Joho, lakini hatua ya majaji Olga Sewe, Stephen Githinji…

Nassir alenga Kufufua Uchumi wa Mombasa
FARAAN:Mbunge wa Mvita Bw Abdulswamad Nassir ambaye anagombea ugavana kaunti ya Mombasa kwa tiketi ya ODM, amewahakikishia wawekezaji wa utalii kuwa atafufua sekta hiyo kwa kupunguza ada za mahoteli na leseni. Alisema uchumi wa Mombasa lazima ufufuliwe kupitia sekta ya utalii. “Tutahakikisha washikadau wanafanya biashara bila ya kuhangaishwa, serikali yangu itashirikiana na mwekezaji ambaye ataweza…

Wanasiasa jijini Mombasa Waahidi Kufanya Kampeni Kwa Amani
Wagombea ugavana na viti vingine vya kisiasa katika Kaunti ya Mombasa, wametia sahihi makubaliano mbele ya viongozi wa dini kwamba watadumisha amani katika kipindi chote cha uchaguzi wa Agosti. Mkataba huo wa Amani, uliandaliwa na Baraza la Kitaifa la Makanisa ya humu nchini (NCCK), Baraza kuu la Waislamu nchini (SUPKEM), Kongamano la Mapadri wa Kikatoliki…

Sonko, Nassir Kukutana Ana Kwa Ana Hafla Ya Azimio Tononoka
ALIYEKUWA Gavana wa Nairobi, Bw Mike Sonko, ameapa kuhudhuria mkutano wa hadhara unaotarajiwa kuongozwa na kinara wa ODM, Bw Raila Odinga, katika uwanja wa Tononoka ulio Mombasa kesho Jumamosi. Iwapo mkutano huo utafanyika ilivyopangwa, itakuwa ni mara ya kwanza Bw Sonko kukutana hadharani na Mbunge wa Mvita, Bw Abdulswamad Nassir, ambao wote ni wagombeaji ugavana…

Hassan Joho afifia kisiasa
USHAWISHI wa Gavana wa Mombasa, Bw Hassan Joho, kwa siasa za Pwani na kitaifa kwa jumla umekosekana kwa takriban wiki mbili sasa baada ya kuugua kwake. Ilibainika Bw Joho alianza kuugua punde alipowasili nchini kutoka ziara ya Uingereza ambapo alikuwa ameandamana pamoja na Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na wanasiasa wengine wa Muungano wa…