
Wapalestina 2 wauawa shahidi, Mzayuni aangamizwa Ukingo wa Magharibi
Jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel limewaua shahidi vijana wawili wa Kipalestina kwa kuwapiga risasi kaskazini mwa eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu. Jeshi la Israel limesema katika taarifa kuwa, Wapalestina hao wawili wameuawa mapema leo katika kituo cha upekuzi wa usalama karibu na kijiji cha Jalamah, kaskazini mwa…

Mateka 73 wa Kipalestina wafa shahidi katika jela za utawala wa Kizayuni kwa kukosa matibabu
Taasisi ya kutetea haki za binadamu ya Palestina imetangaza kuwa, tangu mwaka 1967 hadi sasa Wapalestina 73 wameaga dunia kutokana na upuuzaji unaofanywa na Israel wa kutowapatia matibabu stahiki mateka wa Kipalestina katika jela za utawala huopandikizi unaozikalia kwa mabavu ardhi za Palestina. Klabu ya wafungwa ya Palestina jana Jumapili imeripoti kuwa, raia hao 73…

Jeshi la Israel lakiri kuwa katika wakati mgumu wa kukabiliana na operesheni za wanamapambano wa Kiislamu
Baadhi ya duru za Kizayuni zimeripoti kuwa, licha ya jeshi la Israel kuvamia kila siku na mara kwa mara maeneo ya Wapalestina na licha ya kufanya ukatili mkubwa dhidi ya Wapalestina lakini limeshindwa kuzuia operesheni za wanamuqawama na wanamapambano wa Kiislamu. Shirika la habari la Kizayuni la “Walla” limewanukuu baadhi ya maafisa wa kijeshi wa…

Jihadul Islami: Jinai za Israel zinazidisha ari na irada ya muqawama
Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina imetangaza kuwa, jinai za utawala ghasibu wa Israel zinazidisha ari na irada ya muqawama na mapambano ya Wapalestina dhidi ya utawala huo ghasibu. Taarifa iliyotolewa na Harakati ya Jihadul-Islami imepongeza operesheni ya kimuqawama ya Wapalestina katika ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan iliyopelekea kujeruhiwa wanajeshi saba wa Israel na kueleza kwamba,…

Hamas: Mauaji ya raia wa Kipalestina yanaonesha sura mbaya ya Israel
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kuwa, mauaji yanayofanywa kwa makusudi na askari wa Israel dhidi ya raia wa Kipalestina yanaonyesha sura mbaya ya wavamizi hao wanaoikalia Palestina kwa mabavu. Katika mahojiano yake na kituo cha redio cha Saut al-Aqsa, Fouzi Barhoum ameongeza kuwa, matamshi yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa…

Mamlaka ya Ndani ya Palestina: Matamshi ya karibuni ya Lapid ni sawa na kutoa kibali cha kuuliwa Wapalestina
Wizara ya Mambo ya Nje ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imesisitiza kuwa utawala wa Kizayuni unabeba dhima ya kuwa masuuli wa jinai zinazofanywa kwa Wapalestina, kukiukwa haki za raia hao, ardhi na matukufu ya Palestina kwa hatua yake ya kuwaunga mkono kikamilifu wauaji, watenda jinai, na magaidi wake. Wazayuni maghasibu kila siku huvamia na…

Baraza la Wanazuoni Wataalamu: Palestina ndio kadhia ya kwanza ya ulimwengu wa Kiislamu
Baraza la Wanazuoni Wataalamu linalomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na kusimamia kazi zake limesisitiza kuwa, Palestina ndio kadhia ya kwanza katika ulimwengu wa Kiislamu kama ilivyo pia suala la Beitul-Muqaddas. Sisitizo hilo limo katika taarifa ya mwisho ya mkutano wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu linalomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya…

Wanajeshi wa Israel wamuua kijana Mpalestina katika Ukingo wa Magharibi
Vikosi vya kijeshi vya utawala ghasibu wa Israel vimempiga risasi na kumuua shahidi kijana mwingine wa Kipalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo siku ya Jumatatu. Mpalestina huyo aliyekuwa na umri wa miaka 19 alipigwa risasi na kuuawa na jeshi la Israel wakati wa uvamizi mapema Jumatatu huko Qabatiya, kusini mwa…