
Ziyad al-Nakhala: Katu hatutasalimu amri; adui anataka kutufanya watumwa
Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina amesisitiza kuwa, katu wananchi wa Palestina hawatasalimu amri mbele ya adui Mzayuni na kwamba, bendera ya Palestina itaendelea kupepea. Ziyad al-Nakhala, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina amebainisha kuwa, lengo la adui ni kutufanya watumwa hivyo katu hatuwezi kusalimu amri. Kiongozi huyo mwandamizi wa Harakati ya…

Wanajeshi wa Israel waendeleza jinai katika maeneo tofauti ya Palestina
Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wanaendelea na jinai zao dhidi ya Wapaelstina katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Kanali ya Telegram ya al Risala imesambaza mkanda wa video leo Jumanne unaoonesha jinai za wanajeshi makatili wa Israel na jinsi wanavyovamia na kufanya ukatili dhidi ya Wapalestina katika mji wa al Khalil wa…

Hamas yaishukuru Iran kwa kuunga mkono ukombozi wa Palestina
Afisa mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuunga mkono harakati za ukombozi wa Palestina. Mahmoud al-Zahar ameyasema hayo Jumatatu katika mahojiano na Radio ya Al Aqsa. Amesema Iran imekuwa ikiunga mkono harakati dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unakalia kwa mabavu ardhi…

Zaidi ya nusu karne sasa tangu kufanyika jinai ya kuchomwa moto Msikiti wa al-Aqswa
Jumapili ya jana tarehe 21 Agosti ilisadifiana na kutimia mwaka wa 53 tangu kuchomwa moto Msikiti mtakatifu wa al-Aqswa, kibla cha kwanza cha Wiaslamu, jinai ambayo ilifanywa na utawala vamizi wa Israel ambapo walimwengu walibakia kuwa watazamaji tu na kutoonyesha radiamali yoyote kwa kitendo hicho cha kinyama. Tarehe 21 Agosti 1969 Mzayuni mmoja aliuchoma moto…

Wafungwa wa Palestina waanza mgomo wa kula
Mateka wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za kuogofya za utawala wa Kizayuni wa Israel wameanzisha mgomo usio na kikomo wa kula chakula. Shirika la habari la Palestin al-Yaum limeinukuu Bodi ya Wafungwa Wapalestina ikisema kuwa, hali ya taharuki imetanda katika jela na magereza ya utawala wa Kizayuni, baada ya mateka hao wa Kipalestina kuanza mgomo…

Siku ya Kimataifa ya Misikiti; Palestina iko mstari wa mbele kulinda Msikiti wa al Aqsa
Khatibu wa Msikiti wa al Aqsa katika mji mtakatifu wa Quds huko Palestina amesema kuwa, Msikiti huo mtakatifu bado uko kwenye moto wa jinai za Wazayuni lakini wananchi wa Palestina wataendelea kuwa mstari wa mbele kuulinda. Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu ya Palestina OIC imeitangaza tarehe 21 Agosti kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Misikiti…

Sheikh Ikrima Sabri: Quds na Msikiti wa al-Aqswa vinapitia kipindi kigumu
Khatibu wa msikiti mtakatifu wa al-Aqswa huko Palestina amesema kuwa, Quds na Msikiti wa al-Aqswa vinapitia kipindi kigumu kabisa. Sheikh Ikrima Sabri amesema kuwa, moto katika Msikiti mtakatifu wa al-Aqswa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu bado haujazimika. Akizungumza kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka ambao Wazayuni walikichoma moto Kibla cha Kwanza cha Waislamu…

Uhusiano wa Uturuki na Israel walipiga jambia kwa nyuma taifa la Palestina
Kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa Harakati ya Ukombozi wa Wananchi wa Palestina amelaani vikali hatua ya Uturuki ya kurejesha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel. Jumatano iliyopita, Uturuki na utawala wa Kizayuni zilikubaliana kufufua uhusiano baina yao baada ya kusimama kwa muda wa miaka minne. Mwaka 2018 Uturuki ilisimamisha uhusiano…