
Sisitizo la Kiongozi Muadhamu kuhusu kuinuliwa hadhi ya Harakati ya Jihad Islami
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amejibu barua ya Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina na kusema, “mapambano (muqawama) ya kishujaa ya Jihad Islami yatapelekea kupanda hadhi ya harakati hiyo katika mapambano sambamba na kusambaratisha hadaa za utawala wa Kizayuni na kuufedhehesha utawala huo.” Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi…

Israel imewaua shahidi watoto Wapalestina zaidi ya 1,000 tangu 2008
Tangu mwaka 2008, zaidi ya watoto elfu moja wa Kipalestina wameuawa shahidi katika Ukanda wa Gaza katika mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel Kwa mujibu wa kanali ya televisheni ya Al-Mayadeen siku ya Alkhamisi, mashahidi 15 kati ya 43 wa mashambulizi ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza…

Jibu la Kiongozi Muadhamu kwa Barua ya Katibu Mkuu wa Jihad Islami ya Palestina
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amejibu barua ya Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina na kusema, “mapambano (muqawama) ya kishujaa ya Jihad Islami yatapelekea kupanda hadhi ya harakati hii katika mapambano sambamba na kusambaratisha hadaa za utawala wa Kizayuni na kuufedhehesha utawala huo.” Kwa mujibu wa taarifa ya tovuti ya Ofisi…

Je, ni nani mshindi hasa wa vita vya siku tatu huko Gaza?
Ikiwa ni katika kueneza siasa zake za kipropaganda, utawala wa Kizayuni wa Israel unaeneza uongo kuwa mara hii harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS haikushirikiana na harakati ya Jihad Islami katika vita vya siku tatu vya hivi karibuni huko Katika Ukanda wa Gaza. Lakini ukweli wa mambo ni kwamba utawala huo unapuuza kwa…

Wairani waandamana kulaani ukatili wa Israel dhidi ya wakazi wa Gaza
Wananchi wa Iran jana Jumanne walifanya maandamano katika mji mkuu Tehran kulaani jinai za utawala wa Kizayuni za kuwaua shahidi wanawake na watoto wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza. Maelfu ya waandamanaji walioshiriki kwenye maandamano hayo walikusanyika katika Medani ya Palestina jijini Tehran, karibu na ubalozi wa Palestina nchini Iran huku wakiwa wamebeba bendera za…

AU yalaani ukatili wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza
Umoja wa Afrika (AU) umeungana na jamii ya kimataifa kulaani jinai za kinyama zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Ukanda wa Ghaza huko Palestina. Katika taarifa jana Jumapili, Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU, Moussa Faki Mahamat amesema kushambuliwa raia na kuendelea kukaliwa kwa mabavu maeneo ya Palestina na…

Raia Wapalestina 45 wameuawa shahidi katika siku 3 za hujuma za kikatili za Israeli huko Gaza
Siku tatu za mashambulizi ya utawala haramu wa Israel huko Gaza yamesababisha vifo vya raia Wapalestina 45 wakiwemo watoto 15 na wanawake wanne huku wengine 360 wakijeruhiwa Hayo yameripotiwa baada ya mapatano ya usitishaji vita kutangazwa kuanzia saa tano usiku jana Jumapili kwa saa za Gaza (20:30 GMT). Tangu Ijumaa, utawala wa Kizayuni wa Israel…

Watoto 6 ni katika Wapalestina 24 waliouliwa kikatili na Wazayuni tangu Ijumaa
Idadi ya Wapalestina waliouliwa shahidi katika jinai zinazoendelea za utawala wa Kizayuni huko Ghaza imeongezeka na kufikia watu 24 wakiwemo watoto wadogo sita. Utawala katili wa Israel unaoua watoto wadogo bila kiwewe, ulianzisha mashambulizi makubwa juzi Ijumaa dhidi ya maeneo ya makazi ya watu huko Ghaza na hadi leo Jumapili, mashambulio hayo yanaendelea. Wizara ya…