Wapalestina 6 wapigwa risasi na kujeruhiwa katika ukatili mpya wa Wazayuni
Wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewapiga risasi na kuwajeruhi Wapalestina sita wakati walipovamia maeneo tofauti ya Wapalestina hao katika maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Baraza jipya la mwaziri la Benjamin Netanyahu lilianza kazi rasmi tarehe 29 Disemba 2022. Wataalamu wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa, serikali hiyo mpya…
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena lataka mtazamo wa Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu kuhusu Palestina
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kwa kupitisha azimio, limetaka maoni ya ushauri ya Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) kuhusu namna utawala ghasibu wa Israel unavyokiuka haki ya Wapalestina ya kujitawala na kujiainishia hatima na utawala wao. Katika azimio hilo, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu itoe rai au…
Mfalme wa Jordan aonya: Intifadha mpya ya Wapalestina inanukia
Mfalme wa Jordan ameonya kuhusiana na hatua za utawala haramu za Israel za kushadidisha mivutano na jinai dhidi ya Wapalestina na kueleza kuwa, jinai hizo huenda zikapelekea kuibuka Intifadha mpya ya Wapalestina. Mfalme Abdullah II wa Jordan amesema hayo katika mahojiano na televisheni ya CNN na kutahadharisha kuhusiana na hatari ya kushadidi hatua za uchochezi na kuzusha…
Haniya: Wapalestina watashadidisha mapambano dhidi ya ujenzi haramu wa Israel
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ameionya Israel dhidi ya sera yake ya unyakuzi wa ardhi na kusisitiza kuwa, ujenzi wa vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni utakabiliwa kwa nguvu kupitia muqawama. Ismail Haniya amesema hayo leo Alkhamisi akijibu matamshi yaliyotolewa na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu ajaye wa…
Shtayyeh: Wapalestina 220 wameuawa shahidi mwaka huu wa 2022
Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema: Tangu mwanzoni mwa mwaka huu utawala wa Kizayuni wa Israel umewaua shahidi Wapalestina zaidi ya 220 katika maeneo tofauti ya Palestina. Akizungumza katika kikao cha kila wiki cha Baraza la Mawaziri la Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mohammad Shtayyeh, Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya…
Israel yawaweka mamia ya watoto wa Kipalestina katika kifungo cha nyumbani
Kamisheni ya Wafungwa wa Kipalestina imesema utawala haramu wa Israel umewaweka watoto zaidi ya 600 wa Kipalestina katika kifungo cha nyumbani, tokea mwanzoni mwa mwaka huu hadi sasa, huku utawala huo wa Kizayuni ukiendelea na kampeni yake ya kuwanyanyasa na kuwatia mbaroni Wapalestina. Tume hiyo ya kupigania maslahi ya wafungwa wa Kipalestina imesema katika taarifa ya…
Erdogan: Ronaldo alikalishwa benchi Kombe la Dunia kutokana na uungaji mkono kwa Palestina
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amedai kuwa nyota wa soka wa Ureno Cristiano Ronaldo alipigwa marufuku ya kisiasa wakati wa michuano ya Kombe la Dunia ya FIFA ya 2022 iliyomalizika hivi karibuni nchini Qatar kwa kuunga mkono Palestina. Akizungumza katika hafla na vijana katika jimbo la Erzurum mashariki mwa nchi hiyo siku ya Jumapili,…
2022; mwaka wa muqawama wa Palestina
Ahmed al Mudallal, mmoja wa viongozi waandamizi wa Harakati ya Jihad al Islami ya Palestina amesema kuwa, bila ya shaka yoyote mwaka 2022 umekuwa ni mwaka wa mafanikio makubwa ya muqawama wa Palestina. Al Mudallal ametoa ushahidi kadhaa wa kuthibitisha kuwa mwaka wa 2022 ambao uko ukingoni tena kumalizika, umekuwa ni mwaka wa mafanikio makubwa…