
Wapalestina 160 wameuawa shahidi tangu kuanza mwaka huu
Kwa akali Wapalestina 160 wameuawa shahidi na jeshi la utawala haramu wa Israel katika ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan tangu kuanza mwaka huu wa 2022. Sambamba na mauaji hayo, wanajeshi wa Israel wakishirikiana na walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakifanya hujuma katika maeneo mbalimbali ya Wapalestina kwa ajili ya kusukuma mbele mpango mchafu wa kujitanua…

‘Arin al Usud: Tumefanya operesheni 5 za kulipiza kisasi dhidi ya Wazayuni
Kundi la mapambano ya Kiislamu la ‘Arin al Usud (Pango la Simba) linaloendesha mapambano yake katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina limetoa taarifa na kusisitiza kuwa limefanya operesheni tano za kulipizia kisasi cha kuuliwa shahidi na kikatili kijana wa Kipalestina, Ammar Mefleh. Taarifa ya kundi hilo la muqawama wa Kiislamu imesema kuwa,…

Sheikh Ali Da’mush: Mshindi halisi wa Kombe la Dunia Qatar ni Palestina
Naibu wa Mkuu wa Baraza la Utendaji la Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, mshindi halisi wa fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini Qatar ni taifa la Palestina kutokana na wimbi kubwa la wachezaji na mashabiki wa soka kuwaunga mkono wananchi wa Palestina. Sheikh Ali Da’mush amebainisha kuwa, matukio mbalimbali yanayoshuhudiwa hivi sasa katika mashindano…

Kimya cha jamii ya kimataifa na kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina
Mashambulizi ya Wazayuni dhidi ya raia wa Palestina yanaendelea katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu katika kivuli cha kimya na upuuzaji wa jamii ya kimataifa. Mashambulizi ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni yameshtadi katika miezi kadhaa ya karibuni katika maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan hasa katika miji ya Jenin na…

Wazayuni wameshaua shahidi Wapalestina 205 tangu mwanzoni mwa 2022
Wizara ya Afya ya Palestina imetoa ripoti yake na kusema kuwa, tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2022 hadi hivi sasa, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshaua shahidi Wapalestina 205 katika sehemu mbalimbali za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni. Wizara ya Afya ya Palestina aidha imesema kwenye ripoti yake hiyo ya jana Jumanne kwamba,…

Kanali ya Kizayuni: Israel inakabiliwa na Intifadha mpya ya Wapalestina
Chombo kimoja cha habari cha Kizayuni kimesema hali ya usalama katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu ni ya ‘hatari’ na kwamba Tel Aviv inakabiliwa na Intifadha mpya ya Wapalestina. Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Kanali ya 12 ya Kizayuni, tangu kuanza kwa operesheni za hivi karibuni katika…

Wapalestina pawatatu wakiwemo ndugu wawili wa kiume wauliwa shahidi Ukingo wa Magharibi
Wapalestina watatu wakiwemo ndugu wawili wa kiume Jawaad na Dhaafar Abdurrahman wameuawa shahidi asubuhi ya leo baada ya kupigwa risasi na askari katili wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika kijiji cha Kafr Ain kaskazini mwa Ramallah, Ukingo wa Magharibi Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Duru za Palestina zimeripoti kuwa Dhaafar Abdurrahman Rimawi mwenye umri…

Jumuiya 198 za Palestina na za kimataifa zatoa mwito kwa ICC kuchunguza jinai za Israel
Makumi ya asasi za Palestina na za kimataifa zimeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ifanye uchunguzi kuhusu jinai zinazofanywa na Wazayuni dhidi ya wananchi wa Palestina. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na Falastin al-Yaum, jumuiya 198 za Palestina na za kimataifa zimemtaka Karim Khan, Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai na…