
Ziara ya kiduru ya Lavrov katika nchi za Afrika; jitihada za Russia za kuzidisha satwa yake barani Afrika
Sergei Lavrov Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Jumatatu tarehe 23 mwezi huu alianza safari ya kiduru kwa kuzitembelea nchi kadhaa za Kiafrika na hadi sasa amefanya safari huko Afrika Kusini, Eswatini, Angola na Eritrea. Hii ni safari ya pili kufanywa na Lavrov barani Afrika katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Waziri wa Mambo…

Israel yaufyata baada ya onyo la Russia, yakataa ombi la US la kuipa Ukraine makombora
Utawala haramu wa Israel umepinga ombi la Marekani la kuutaka uipe Ukraine makombora na silaha nyinginezo, baada ya Russia kuonya vikali dhidi ya kupewa Kiev misaada ya kijeshi na zana za vita. Tovuti ya Russia Today imeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, duru za habari zimenukuliwa na shirika la habari la Axio zikisema kuwa, Israel…

Balozi: Marekani inashajiisha vitendo vya kigaidi dhidi ya Russia
Balozi wa Russia nchini Marekani ameonya vikali dhidi ya mashambulizi tarajiwa ya Ukraine katika Peninsula ya Crimea na kusisitiza kuwa, Moscow itajibu mapigo baada ya Washington kudokeza kuwa huenda Kiev ikatumia silaha za Magharibi kulishambulia eneo hilo. Akitoa radiamali yake kwa kauli ya hivi karibuni ya Ned Price, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje…

Ushirikiano wa kiuchumi wa Iran na Russia unaenda sambamba na makubaliano ya kimkakati
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Kitaifa la Iran amesema Tehran na Moscow zinaimarisha ushirikiano wao wa kiuchumi kwa mujibu wa makubaliano ya kimkakati kupitia juhudi za mara kwa mara na azma thabiti. Ali Shamkhani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Kitaifa la Iran aliyasema hayo Jumanne na kuongeza kuwa ni muhimu kwamba…

Umoja wa Mataifa na jitihada za kuondoa vizuizi kwa usafirishaji wa mbolea ya Russia
Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa umoja huo unajaribu kila linalowezekana kuondoa vizuizi vinavyokwamishwa usafirishaji wa mbolea ya Russia. Stephane Dujarric Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kuhusu kusafirishwa mbolea ya Russia kufuatia vita vinavyoendelea huko Ukraine kwamba, Katibu Mkuu Antonio Guterres na viongozi wengine wa umoja huo wanaendelea kufanya juhudi ili kuondoa vizuizi…

Putin atuma manowari yenye makombora ya hypersonic Bahari ya Atlantic, Hindi
Rais Vladimir Putin wa Russia ameagiza kutumwa katika Bahari ya Atlantic na Bahari Hindi meli ya kivita iliyosheheni makombora ya hypersonic huku vita vya Ukraine vikipamba moto. Rais Putin jana Jumatano kupitia njia ya video, alishiriki katika hafla ya kuiaga manowari hiyo ya kijeshi ya ‘Admeli Gorshkov’ kuelekea Bahari ya Atlantic na Bahari Hindi. Sergei Shoigu, Waziri wa Ulinzi…

Putin: Hatutaruhusu Magharibi kuisambaratisha Russia
Rais wa Russia ametangaza kuwa Moscow haitaziruhusu nchi za Magharibi kuwatumia watu wa Ukraine kwa ajili ya kuigawa na kuidhoofisha Russia. Katika hotuba yake ya kufunga mwaka wa 2022, Rais wa Russia, Vladimir Putin ameutaja mwaka uliomalizika wa 2022 kuwa ulikuwa mwaka uliojaa matukio ambayo ni msingi wa mustakabali wa uhuru na kujitawala kikamilifu nchi yake. Kuhusu…

Russia kuipa Iran idadi kubwa ya ndege za kivita za kisasa aina ya Sukhoi Su-35
Hivi karibuni Russia inatazamiwa kuipatia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndege za kivita aina ya Sukhoi Su-35 hatua ambayo yumkini ikazikasirisha zaidi nchi za Magharibi kutokana na ushirikiano wa kijeshi unaozidi kuimarika kati ya Tehran na Moscow. Ripoti za vyombo vya habari, zikiwanukuu wataalamu wa kijeshi, Iran itapokea ndege 24 za kivita za Sukhoi Su-35…