
Moscow yatoa onyo baada ya Washington kutishia kumuua Rais wa Russia
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ametoa indhari baada ya maafisa ‘wasiojulikana’ wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) kutoa vitisho vya kumuua Rais Vladimir Putin wa nchi hiyo. Katika mahojiano na shirika la habari la TASS, Sergei Lavrov amesema, “Washington imekubuhu, maafisa wasiojulikana wa Washington wamepaza sauti na kutishia kuishambulia vikali Kremlin (Ikulu…

Russia yapeleka manowari 3 za kubebea makombora Bahari Nyeusi
Russia imepeleka manowari tatu za kubebea makombora katika Bahari Nyeusi na kuziweka meli hizo za kivita katika hali ya tahadhari. Duru za habari zinaarifu kuwa, manowari hizo za kijeshi zimesheheni makombora 20 aina ya Kalibr. Kwa mujibu wa Waziri wa Ulinzi wa Russia, Sergei Shoigu, kombora moja la Kalibr linaweza kubeba kichwa cha nyuklia chenye uzani wa…

Russia: Jinai za kivita za Marekani na Nato Afghanistan zimepuuzwa
Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema katika kikao cha Baraza la Usalama la umoja huo kuwa jinai za kivita za Marekani na Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (Nato) huko Afghanistan zimepuuzwa. Marekani na waitifaki wake Oktoba 7, 2001 ziliivamia na kuanza kuikalia kwa mabavu Afghanistan kwa kisingizio cha kupambana…

Erdogan: Borrell hana mamlaka ya kuzungumzia uhusiano wa Uturuki na Russia
Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema: Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya hana mamlaka ya kuzungumzia uhusiano wa Uturuki na nchi zingine ikiwemo Russia. Erdogan amesema matamshi aliyotoa hivi karibuni Joseph Borrell, Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya kuhusu uhusiano wa Ankara na Moscow ni za kuchukiza na…

Mkutano wa 18 wa kimataifa wa nchi za Kiislamu wafunguliwa Russia kwa salamu za Rais wa Iran
Mkutano wa 18 wa kimataifa unaofanyika kwa anuani ya “Uislamu, Uadilifu na Mlingano, Misingi ya Dini na Nidhamu ya Ulimwengu” umeanza rasmi katika mji mkuu wa Russia, Moscow na kufunguliwa kwa salamu za Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB, zaidi ya shakhsia…

Vitisho vya ajabu vya Marekani kwa Russia; ukiacha kutuuzia mafuta tutakuadhibu
Msemaji wa Ikulu ya Marekani, White House mapema leo Jumanne ametoa vitisho vya ajabu dhidi ya Moscow baada ya nchi za Magharibi kuainisha bei maalumu ya kununulia mafuta ya Russia, na kusema kuwa hakushangazwa na radiamali iliyooneshwa na Kremlin. Shirika la habari la FARS limemnukuu Karine Jean-Pierre akisema hayo mapema leo na kuongeza kuwa, iwapo Russia…

Ulyanov: Ulaya ifikirie kuishi bila ya mafuta ya Russia
Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika taasisi za kimataifa mjini Vienna, Austria amesema kuwa, kuanzia mwaka ujao Ulaya itaishi bila ya mafuta ya Russia kufuatia hatua yake ya kuainisha bei ya mafuta kutoka Russia. Mikhail Ulyanov ametoa matamshi hayo akijibu hatua ya nchi za Magharibi na Umoja wa Ulaya ya kuianisha bei ya dola 60…

Russia: Hakuna ushahidi Iran inataka kuunda silaha za nyuklia
Afisa mmoja wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema hakuna ithibati wala ushahidi wowote unaoashiria kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inataka kuzalisha silaha za nyuklia au kutazama upya uanachama wake katika Mkataba wa Kuzuia Uzalishaji na Uenezaji wa Silaha za Nyuklia NPT. Vladimir Yermakov, Mkurugenzi wa Idara ya Kuzuia Uenezaji wa Silaha za…