#russia

Russia, Uchina zalaani ‘matumizi ya nguvu kupita kiasi’ ya Israel dhidi ya Wapalestina

Russia, Uchina zalaani ‘matumizi ya nguvu kupita kiasi’ ya Israel dhidi ya Wapalestina

Russia na China zimeulaani vikali utawala wa Israel kutokana na utumiaji wake mabavu kupita kiasi dhidi ya Wapalestina huku hali ya wasiwasi ikiongezeka katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu. Akizungumza katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Mashariki ya Kati, likiwemo suala la Palestina, siku ya Jumatatu, naibu balozi wa…

Moscow yajibu mpango wa CIA wa kuwasajili raia wa Russia

Moscow yajibu mpango wa CIA wa kuwasajili raia wa Russia

Ubalozi wa Russia mjini Washington umesema azma ya Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) ya kutaka kuwasajili raia wa Russia katika taasisi hiyo ni ithibati nyingine inayoonesha kuwa Marekani inafanya juu chini ili kuidhalilisha nchi hiyo. Hata hivyo ubalozi huo umesisitiza kuwa njama hizo za Washington hazitafua dafu. Ubalozi huo wa Russia nchini Marekani umesema…

Bunge la nchi wanachama wa NATO lalitangaza shirikisho la Russia ‘dola la kigaidi’

Bunge la nchi wanachama wa NATO lalitangaza shirikisho la Russia ‘dola la kigaidi’

Baraza la mabunge ya nchi wanachama wa shirika la kijeshi la NATO limepitisha azimio ambalo limelitaja shirikisho la Russia kuwa ni ‘dola la kigaidi’. Kwa mujibu wa tovuti ya chaneli ya CNBC, Yehor Chernov, mkuu wa ujumbe wa kudumu wa Ukraine kwenye baraza la mabunge ya nchi wanachama wa NATO, ametangaza katika taarifa kwamba, katika mkutano wake…

Mashindano ya Kimataifa ya Qurani yamalizika Moscow, Russia

Mashindano ya Kimataifa ya Qurani yamalizika Moscow, Russia

Duru ya 20 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qurani Tukufu iliyoanza Ijumaa iliyopita katika mji mkuu wa Russia, Moscow imemalizika huku washindi wakitangazwa na kutuzwa. Raia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Mostafa Hosseini ameibuka mshindi wa tatu kwenye mashindano hayo ya dunia yaliyofanyika katika Msitiki wa Jamia jijini Moscow. Nafasi ya kwanza imetwaliwa na…

Russia na China zapinga azimio la Bodi ya Magavana ya Wakala wa IAEA dhidi ya Iran

Russia na China zapinga azimio la Bodi ya Magavana ya Wakala wa IAEA dhidi ya Iran

Azimio jipya la Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) dhidi ya miradi ya nyuklia ya Iran yenye malengo ya amani limepasishwa ambapo limetuma ujumbe ulio wazi kufuatia kupungua kwa kura za nchi zilizoliunga mkono licha ya mashinikizo mapya ya kisiasa ya Marekani na Troika ya Ulaya dhidi ya Iran….

Russia: Kilichotokea Poland ni ithibati kuwa Magharibi inakaribia zaidi kuanzisha Vita vya Dunia

Russia: Kilichotokea Poland ni ithibati kuwa Magharibi inakaribia zaidi kuanzisha Vita vya Dunia

Naibu Mkuu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Russia ametahadharisha juu ya kuzuka vita vya dunia kufuatia tuhuma zilizotolewa na Magharibi dhidi ya Moscow katika tukio la kombora lililoangukia ndani ya ardhi ya Poland. Radio Zeit ya Poland ilitangaza jana usiku kuwa makombora mawili yamepiga kijiji cha Przewodów katika eneo la Lobelski Voivodeship mashariki mwa…

Marekani yaitaka Ukraine ifanye mazungumzo ya amani na Russia

Marekani yaitaka Ukraine ifanye mazungumzo ya amani na Russia

Maafisa wa ngazi za juu wa Marekani wameanzisha kampeni ya kuishawishi Ukraine itafakari juu ya suala la kufanya mazungumzo ya amani na Russia, wakihofia kuwa msimu wa baridi kali yumkini ukaikwamisha serikali ya Kiev baada ya eti kupata ushindi wa kulidhibiti tena eneo la Kherson. Gazeti la The Wall Street Journal la Marekani limeripoti kuwa,…

Onyo la Russia kuhusu Wamagharibi kutuma magaidi nchini Ukraine

Onyo la Russia kuhusu Wamagharibi kutuma magaidi nchini Ukraine

Katibu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Russia, Nikolay Patrushev, ametangaza kuwa Marekani na Uingereza zinasajili na kuajiri magaidi wa kimataifa kwa ajili ya kushirikiana na jeshi la Ukraine katika vita dhidi ya Russia. Patrushev, ambaye alikuwa akizungumza katika mkutano wa makatibu wa Baraza la Usalama la Jumuiya ya Madola Huru (CIS) siku ya…