Dar es Salaam. Wakati wagonjwa wa saratani wakiongezeka nchini, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) imesema kati ya wagonjwa wapya 8,000 na wale wa marudio 68,000 waliopokelewa mwaka 2021 asilimia 70 ni wanawake. Licha ya saratani ya kizazi na ile ya matiti zinazowahusu wanawake kuongoza, imeelezwa kuwa wanawake pia wamekuwa wakiathirika kwa kiasi kikubwa katika…