
Bin Salman anaigeuza ardhi ya maeneo matakatifu ya Makka na Madina uwanja wa ufasiki wa kimaadili
Mwandishi wa habari na mpinzani wa utawala wa kifalme wa Saudi Arabia amekosoa kufanyika tamasha la muziki liitwalo MDLBEAST katika ardhi ya maeneo mawili matakatifu (Haramaini-Sharifaini) ya Makka na Madina na kueleza kwamba: Bin Salman anatoa huduma kubwa zaidi kwa maadui wa Uislamu kwa kuigeuza nchi hiyo kuwa uwanja wa kufanyia ufisadi wa kimaadili. Katika…

Bin Salman asherehekea Siku ya Wanawake kwa kutia mbaroni wanaharakati 100 wa kike
Shirika la Haki za Binadamu la Sanad limesema kuwa, viongozi wa Saudi Arabia wamewatia mbaroni makumi ya wanaharakati wa kike wanaopigania haki za wanawake nchini humo sambamba na maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Ukatili dhidi ya Wanawake. Utawala wa kiimla wa Saudia unaendelea kukanyaga vibaya haki za wanawake. Kwa mujibu wa ripoti…

Bin Salman na Bin Zayed hawana ubavu isipokuwa wa kuua watoto wa Kiyemen
Kadiri siku zinavyosonga mbele ndivyo faili la jinai za kivita la Muhammad bin Salman mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia na Sheikh Muhammad bin Zayed Al-Nahyan Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) huko nchini Yemen linavyozidi kuwa kubwa. Licha ya vyombo vingi vya habari vya Magharibi kuelekeza macho na masikio yao…

Taasisi ya “Democracy For The Arab World Now” yamkosoa Biden kwa kumpa kinga Bin Salman
Taasisi isiyo ya kiserikali ya “Democracy For The Arab World Now” imekosoa hatua ya Rais Joe Biden wa Marekani ya kumpatia kinga ya kutoshtakiwa mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman. Taasisi hiyo imeitaja hatua hiyo ya Biden kuwa ni natija ya siasa na sheria zisizo sahihi. Mrithi huyo wa kiti…

Kuongezeka maradufu watu wanaokatwa vichwa nchini Saudi Arabia
Serikali ya Saudia inatumia vibaya kimya cha madola makubwa na jamii ya kimataifa, kuzidisha kukata vichwa watu kwa visingizio tofauti kiasi kwamba, idadi ya watu waliotekelezewa adhabu ya kifo na ukoo wa Aal Saud mwaka huu, tayari hivi sasa ni maradufu ya waliokatwa vichwa mwaka jana nchini humo. Baada ya kukatwa vichwa watu wengine wawili,…

Kurejea Saudi Arabia katika mfumo wa ukandamizaji; sura halisi ya bin Salman
Katika miezi ya hivi karibuni Saudi Arabia imeingia katika hatua mpya ya vitendo vya ukatili na ukandamizaji dhidi ya wanaharakati wa kisiasa, kiraia na wa haki za binadamu. Viongozi wa utawala vamizi wa Saudi Arabia wameshadidisha utoaji wa hukumu nzito dhidi ya wanaharakati hao na hivyo kuifanya nchi hiyo kuingia katika mkondo mpya wa kushadidisha…

Msururu wa hukumu za vifo na kunyonga watu kwa halaiki; rekodi ya jinai aliyojiwekea Bin Salman
Shirika la Haki za Kibinadamu la Saudi Arabia lenye makao yake Ulaya limefichua kuwa viongozi wa utawala wa Riyadh wametoa hukumu ya kifo kwa wafungwa 15 walioshtakiwa kwa masuala ya kiitikadi, na kwamba kwa kutolewa hukumu hizo, idadi ya watu walio hatarini kunyongwa nchini humo imefika 53, wanane miongoni mwao wakiwa ni vijana chipukizi na…

Saudi Arabia yatakiwa ikomeshe vitendo vya kuwanyonga kiholela wapinzani
Jumuiya na mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu yameelezea wasiwasi mkubwa yaliyonao kutokana na kuongezeka mno hatua za utawala wa Saudi Arabia za kuwanyonga kiholela wapinzani. Jumuiya hizo zimewatolea mwito viongozi wa Saudia na mamlaka husika katika nchi hiyo ya utawala wa kifalme zikomeshe mauaji na hukumu za kiholela za adhabu ya kifo. Mwito…