#syria

Rais wa Uturuki aikosoa Marekani kwa kuunga mkono ugaidi Syria

Rais wa Uturuki aikosoa Marekani kwa kuunga mkono ugaidi Syria

Rais Recep Tayyep Erdogan wa Uturuki amekosoa hatua ya Marekani ya kuyapa makundi ya kigaidi yaliyopo kaskazini mwa Syria msaada wa fedha na silaha. Shirika la habari la Anadolu limemnukuu Erdogan akisema hayo na kuongeza kuwa, “Marekani inatuma malori 4,000-5,000 ya silaha na zana za kijeshi kaskazini mwa Syria. Ingawaje tumewaambia hili mara chungu nzima, lakini hawajali.”…

Bunge la Waarabu lalaani hatua ya Uturuki ya kuwakatia maji raia milioni moja wa Syria

Bunge la Waarabu lalaani hatua ya Uturuki ya kuwakatia maji raia milioni moja wa Syria

Muungano wa Mabunge ya Nchi za Kiarabu umelaani hatua ya Uturuki ya kuwakatia maji raia zaidi ya milioni moja wa Syria katika mkoa wa al-Hasakah. Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Muungano wa Mabunge ya Nchi za Kiarabu umetoa taarifa na kutangaza kuwa, kuendelea hatua ya Uturuki ya kukata maji mara kwa mara nchini…

Hamas yalaani hujuma ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Syria

Hamas yalaani hujuma ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Syria

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ametoa taarifa akilaani mashambulio ya anga ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Syria. Shirika rasmi la habari la Syria (SANA) limeripoti kujiri mashambulizi mapya ya anga ya utawala wa Kizayuni dhidi ya ardhi ya nchi iyo yaliyouwa wanajeshi wanne na kumjeruhi mwingine mmoja….

Tutaendelea na mapambaSyria: Tutaendelea na mapambano dhidi ya ugaidi hadi tutakapoisafisha ardhi yetu yoteno dhidi ya ugaidi hadi tutakapoisafisha ardhi yetu yote

Tutaendelea na mapambaSyria: Tutaendelea na mapambano dhidi ya ugaidi hadi tutakapoisafisha ardhi yetu yoteno dhidi ya ugaidi hadi tutakapoisafisha ardhi yetu yote

Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imetangaza kuwa, mapambano dhidi ya magenge ya kigaidi huko kaskazini na kusini mwa nchi hiyo ya Kiarabu yataendelea hadi kila shibri ya ardhi ya Syria itakaposafishwa kikamilifu. Hayo yamekuja baada ya jeshi la Syria kusambaratisha kambi za mafunzo za magenge ya kigaidi katika mkoa wa Idlib wa kaskazini…

Syria: Tunataka uanzishwe mfumo mpya wa kimataifa, jinai za Israel zidhibitiwe

Syria: Tunataka uanzishwe mfumo mpya wa kimataifa, jinai za Israel zidhibitiwe

Kwa mnasaba wa Siku ya Umoja wa Mataifa, Serikali ya Syria imetoa wito na kusisitiza ulazima wa kuundwa mfumo mpya wa kimataifa na kuzuiwa uchokozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel na jinai zinazofanywa na utawala huo haramu. Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Al-Akhbariya; Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imetoa taarifa…

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq: Ulaya haiko tayari kuwarejesha raia wake wanachama wa Daesh walioko Syria

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq: Ulaya haiko tayari kuwarejesha raia wake wanachama wa Daesh walioko Syria

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iraq amesema kuwa nchi za Ulaya haziko tayari kuwarejesha nyumbani raia wa nchi hizo wanachama wa kundi la Daesh. Daesh na makundi mengine ya kigaidi mwaka 2017 yalisambaratika na kushindwa baada ya miaka minne ya operesheni kubwa za kigaidi huko Syria na Iraq na baada ya kukalia…

Ujumbe wa HAMAS waonana na Rais wa Syria mara ya kwanza baada ya miaka 10

Ujumbe wa HAMAS waonana na Rais wa Syria mara ya kwanza baada ya miaka 10

Duru za Syria zimetangaza habari ya kukutana ujumbe mmoja wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na Rais Bashar al Assad wa nchi hiyo ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. Televisheni ya al Mayadeen ilitangaza habari hiyo jana Jumatano na kuzinukuu duru hizo zikisema kuwa, ujuumbe wa Palestina…

Makumi ya magaidi wa ISIS wauawa katika operesheni ya jeshi la Syria

Makumi ya magaidi wa ISIS wauawa katika operesheni ya jeshi la Syria

Makumi ya wanamgambo wa kundi la kigaidi la ISIS (Daesh) wameangamizwa katika operesheni ya jeshi la Syria kusini mwa nchi. Duru za kiusalama zimeliambia shirika rasmi la habari la Syria SANA kuwa, idadi kubwa ya magaidi wa ISIS wameuawa katika operesheni ya jeshi la Syria likishirikiana na makundi ya kujitolea wananchi katika mkoa wa Dara’a, kusini…