Kipindupindu chazidi kuitesa Malawi; Tanzania yakaa chonjo
Visa vya maambukizi na vifo vitokanavyo na ugonjwa wa kipindupindu nchini Malawi vimezidi kuongezeka huku mikoa ya Tanzania inayopakana na nchi hiyo mikakati ikizidi kuimarishwa ili ugonjwa huo usiingie. Taarifa zaidi zinasema kuwa, idadi ya watu wanaopoteza maisha kwa ugonjwa wa kipindupindu nchini Malawi imezidi kuongezeka kutoka watu 661 hadi kufikia vifo 687. Akizungumza na…
Kongamano la kitaaluma la maulamaa wa Ulimwengu wa Kiislamu lafanyika Tanzania
Kongamano la kitaaluma la wanazuoni wa Ulimwengu wa Kiislamu limefanyika jijini Dar es Salaam kwa kuhudhuriwa na wanafikra kutoka Tanzania na Iran. Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB katika kongamano hilo wahadhiri wa vyuo vikuu na watafiti waliwasilisha makala zenye anuani “umuhimu wa maelewano kati ya wanazuoni wa Ulimwengu wa…
Umoja wa Mataifa wampongeza Samia kwa kuruhusu mikutano ya hadhara ya kisiasa
Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu (OHCHR) imepongeza hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutangaza kuondoa marufuku kwa vyama vya siasa nchini humo kufanya mikutano ya hadhara. Msemaji wa ofisi hiyo kutoka Nairobi, Kenya Seif Magango amesema kuwa, “hatua hii ambayo ameichukua…
Rais Samia: Mikutano ya hadhara ya kisiasa sasa ruhsa Tanzania
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania leo Jumanne, Januari 3, 2022 amekutana na viongozi wa vyama 19 venye usajili kamili wa siasa nchini humo Ikulu jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa, ni haki kwa vyama vya siasa kuendesha mikutano yao ya hadhara nchini humo lakini kuna wajibu wa kila mmoja na upande wa Serikali…
Maulamaa wa Kisunni kutoka Iran wakutana na Mufti wa Tanzania
Ujumbe wa Maulamaa wa Kisunni wa Iran umekutana na kufanya mazungumzo na Mufti wa Tanzania Jumanne. Ujumbe huo kutoka Mkoa wa Golestan kusini mwa Iran, ulikutana na Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry ikiwa ni sehemu ya programu zao nchini Tanzania. Sheikh Salaheddin, mwanzilishi wa Chuo cha Kiislamu cha Chenarli katika mkoa Golestan, amesema lengo…
Mahakama yaamuru mwili uliozikwa 2020 ufukuliwe
Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni (Kinondoni) jijini Dar es Salaam imeamuru mwili wa mwanamke aliyefia mahabusu katika kituo cha Polisi Mburahati wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam, mwaka 2020, Stella Moses ufukuliwe na ufanyiwe uchunguzi kujua chanzo cha kifo chake. Mahama hiyo pia imeamuru matokeo ya uchunguzi huo yawasilishwe katika vyombo husika ili…
Deni la Tanzania lafikia trilioni 91.02 na linaongezeka kila mwezi kwa dola milioni 544
Deni la serikali ya Tanzania linaendelea kuongezeka kila mwezi kwa kiasi cha dola milioni 544.8. Haya yamo katika ripoti ya iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambayo imeeleza pia kuwa, kufikia mwezi Oktoba mwaka huu, Tanzania ilikuwa inadaiwa shilingi trilioni 64 ikiwa ni deni ambalo nchi hiyo inadaiwa na nchi au wafadhili wa nje,…
Mabaharia 16 Wairani waachiliwa huru Tanzania
Mabaharia 16 Wairani waliokuwa wanashikiliwa nchini Tanzania wameachiliwa huru hivi karibuni. Hayo yamedokezwa na Mkuu wa Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran katika Eneo la Biashara Huria la Chabahar katika mkoa wa Sistan na Baluchestan kusini-mashariki mwa Iran ambaye amesema mabaharia hao walioachiliwa huru ni wenyeji wa mkoa wa Sistan na Baluchestan….