Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, unahitajia kiasi cha dola milioni 205 kwa ajili ya misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa jimbo la Tigray. Hayo yameelezwa na Stephane Dujarric, msemaji wa Umoja wa Mataifa katika mkutano wake na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya umoja huo mjini New York na kueleza kwamba, asasi hiyo inahitajia…