Wapiganaji 15 wa ADF wauawa na jeshi la Uganda mpakani na DRC
Askari wa Jeshi la Uganda wamefanikiwa kuwaangamiza wanamgambo 15 wa kundi la waasi la ADF katika mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hayo yalisemwa jana Jumanne na Kanali Deo Akiiki, Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Uganda (UPDF) katika mahojiano na gazeti la The East African na kuongeza kuwa, wapiganaji hao wa ADF waliuawa walipojaribu kuvuka…
Wanandoa wa Marekani waswekwa rumande Uganda kwa kumtesa mtoto wa miaka 10
Mke na mume raia wa Marekani wanaoishi katika mtaa wa Naguru huko Kampala, mji mkuu wa Uganda wametupwa rumande katika gereza la Luzira, wakikabiliwa na mashitaka ya kumtesa na kumdhalilisha mtoto mdogo wa miaka 10. Mackenzie Leing Mathias Spencer na mumuwe Nicholas Spencer wanatuhumiwa kumuadhibu na kumfanyia kila aina ya mateso mtoto wao wa kambo…
Kamata kamata ya Waislamu nchini Uganda yaibua malalamiko
Waislamu nchini Uganda kutoka makundi yote ya jamii jana Jumatatu walipinga kukamatwa kiholela kwa viongozi wa Waislamu wakati wa uvamizi wa misikiti. Viongozi wa dini ya Kiislamu, wabunge, wafanyabiashara na wanajamii kwa pamoja walijitokeza kulaani utiaji mbaroni huo ambao wanaamini ni kinyume cha sheria na haustahili kufanywa. Asuman Basalirwa, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge Waislamu na…
Waziri: Ukimwi unaua Waganda 46 kila siku
Waziri katika Ofisi ya Rais nchini Uganda ameashiria ongezeko la maambukizi ya virusi vya HIV vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi miongoni mwa tabaka la vijana wanaobaleghe nchini humo na kusema kuwa, maradhi hayo yanaua Waganda 46 kwa siku. Milly Babalanda amesema hayo akinukuu takwimu za Wizara ya Afya ya Uganda zinazoonesha kuwa, asilimia 37 ya kesi…
Chanjo tatu za aina adimu ya Ebola ziko tayari huku Uganda ikipambana na mripuko wa ugonjwa huo
Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Shirika la Afya Ulimwenguni WHO amesema kwamba, chanjo tatu za aina adimu ya ugonjwa wa Ebola inayoendelea kusambaa hivi sasa nchini Uganda zitapelekwa nchini humo kwa majaribio ya kizahanati. Dk. Matshidiso Moeti ameaambia waandishi wa habari kwamba chanjo hizo zitatumika katika mfumo unaojulikana kwa kimombo kama “ring vaccination trial”…
Mtoto wa Rais Museveni atangaza kuliunga mkono kundi la waasi wa M23
Mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amesema kwamba kundi la waasi la M23, linalopigana vita na jeshi la serikali ya Kinshasa, lina haki ya kufanya hivyo. Muhoozi ameandika katika ujumbe wa twitter akisema kwamba “ni hatari sana kwa mtu yeyote kupiga vita ndugu zetu. Sio magaidi, bali wanapigania haki za…
Mawaziri wa Uganda waanza kujifunza Kiswahili
Mawaziri wa Uganda wameazimia kuanza kujifundisha lugha ya Kiswahili, ambayo mbali na kuwa lugha ya kitaifa, lakini pia ni lugha rasmi katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Uganda hivi karibuni iliidhinisha Kiswahili kuwa lugha rasmi ya pili nchini humo baada ya Kiingereza, na kuifanya lugha hiyo kuwa ya lazima kufundishwa mashuleni. Makamu wa Kwanza wa…
Benki ya Uganda yazindua akaunti ya kwanza inayofuata sheria za Kiislamu
Benki ya Finance Trust ya Uganda imezindua akaunti ya kwanza kabisa inayofuata sheria za Kiislamu katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Viongozi na shakhsia mbalimbali wa Kiislamu walihudhuria hafla ya uzinduzi wa akaunti hiyo inayoitwa ‘Halal’ jana Alkhamisi katika mji mkuu Kampala. Julai mwaka huu, Baraza la Mawaziri la Uganda liliidhinisha benki za kibiashara za…