#ukraine

Kumalizika ziara ya Zelenskyy nchini Marekani na uwezekano wa kuendelea vita huko Ukraine

Kumalizika ziara ya Zelenskyy nchini Marekani na uwezekano wa kuendelea vita huko Ukraine

Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine amekamilisha ziara yake ya kwanza huko Marekani baada ya kuanza vita huko Ukraine. Hii ni safari ya kwanza nje ya nchi kufanywa na Zelenskyy baada ya kuanza vita huko Ukraine Akiwa ziarani nchini Marekani, Jumatano usiku Zelenskyy alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Joe Biden wa nchi hiyo. Pande mbili…

FIFA yakataa ombi la Rais wa Ukraine la kutangazwa ujumbe wake kabla ya mechi ya fainali

FIFA yakataa ombi la Rais wa Ukraine la kutangazwa ujumbe wake kabla ya mechi ya fainali

Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) inadaiwa limekataa ombi la Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kutaka kabla ya kuchezwa mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia kati ya Argentina na Ufaransa siku ya Jumapili irushwe hewani video yake uwanjani hapo ili kuhamasisha amani. Inadaiwa kuwa Zelensky aliomba hilo huku akitaka kuonekana katika video hiyo akitoa ujumbe…

Askari 13,000 wa Ukraine wameuawa katika vita na Russia

Askari 13,000 wa Ukraine wameuawa katika vita na Russia

Mykhailo Podoliak, mshauri wa Rais wa Ukraine, amesema: vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo hadi sasa vimepoteza kati ya wanajeshi 10,000 hadi 13,000 katika vita dhidi ya Russia. Podoliak amesema katika mahojiano na Channel 24 TV ya Ukraine: “tuna takwimu rasmi kutoka kwa makao makuu ya ya Kamandi ya juu zinazoonyesha idadi hii ya wanajeshi…

Economist: Idadi ya vifo katika majira ya baridi kali Ulaya ni zaidi ya vita vya Ukraine

Economist: Idadi ya vifo katika majira ya baridi kali Ulaya ni zaidi ya vita vya Ukraine

Kwa mujibu wa uchambuzi mpya uliofanywa karibuni, idadi ya watu ambao watapoteza maisha katika msimu wa baridi kali barani Ulaya mwaka huu kutokana na uhaba wa nishati itakuwa zaidi ya wale waliouawa katika vita huko Ukraine. Bei ya nishati ya gesi na umeme kwa ajili ya matumizi ya nyumbani huko Ulaya imeongezeka pakubwa ikiwa ni…

Umoja wa Mataifa: Video za kunyongwa wanajeshi wa Russia huko Ukraine ni za kweli

Umoja wa Mataifa: Video za kunyongwa wanajeshi wa Russia huko Ukraine ni za kweli

Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa ametangaza kwamba kuna uwezekani mkubwa kwamba video za kunyongwa wanajeshi wa Russia waliotekwa nyara huko Ukraine ni za kweli. Kulingana na shirika la habari la IRNA, Volker Türk, Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, amesema katika taarifa yake kwamba matokeo ya…

Onyo la Russia kuhusu Wamagharibi kutuma magaidi nchini Ukraine

Onyo la Russia kuhusu Wamagharibi kutuma magaidi nchini Ukraine

Katibu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Russia, Nikolay Patrushev, ametangaza kuwa Marekani na Uingereza zinasajili na kuajiri magaidi wa kimataifa kwa ajili ya kushirikiana na jeshi la Ukraine katika vita dhidi ya Russia. Patrushev, ambaye alikuwa akizungumza katika mkutano wa makatibu wa Baraza la Usalama la Jumuiya ya Madola Huru (CIS) siku ya…

Baraza la Usalama lakataa kuchunguza maabara za kibiolojia za US Ukraine

Baraza la Usalama lakataa kuchunguza maabara za kibiolojia za US Ukraine

Nchi za Magharibi kwa mara nyingine tena zimelitumia vibaya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kwa kuzuia ombi la Russia la kutaka kufanyika uchunguzi kuhusu uwepo wa maabara za silaha za kibiolojia za Marekani nchini Ukraine. Marekani, Ufaransa na Uingereza zimelipigia veto ombi hilo la Russia, ambalo hata hivyo limeungwa mkono na China. Nchi…

Mashtaka rasmi ya Russia kwa Umoja wa Mataifa kuhusu maabara za silaha za kibiolojia za Marekani nchini Ukraine

Mashtaka rasmi ya Russia kwa Umoja wa Mataifa kuhusu maabara za silaha za kibiolojia za Marekani nchini Ukraine

Russia imepeleka malalamiko yake rasmi kwa Umoja wa Mataifa kuhusu kuwepo kwa maabara za silaha za kibiolojia za Marekani nchini Ukraine. Vasily Nebenzia, ​​mwakilishi wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa, amethibitisha kwamba nchi yake imekusanya ushahidi wa kutosha kuhusu uwepo wa maabara ya silaha hizo za kibiolojia za Marekani huko Ukraine. Kwa kutuma…