Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) na washirika wake wameeleza kushtushwa na ripoti za mashambulizi nane makubwa yaliyotokea katika siku 10 za mwanzo wa mwezi huu wa Februari katika jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Taarifa ya UNHCR iliyotolewa mjini Geneva Uswisi inaeleza kuwa mashambulizi yaliyosababisha watu kuuawa, kutekwa…