Yemen: Tunao uwezo wa kujibu shambulio lolote kwa makombora na droni
Msemaji wa vikosi vya ulinzi vya Yemen, Brigedia Jenerali Yahya Saree amesema vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo vinao uwezo wa kujibu mapigo dhidi ya shambulio lolote lile. Brigedia Saree ameeleza katika taarifa: “huko nyuma, maadui walikuwa wakishambulia Sana’a na mikoa mingine kwa mabomu na makombora bila kujibiwa; lakini leo tunao uwezo wa kujibu shambulio lolote lile kwa…
Ripoti kuhusu jinai za kivita za muungano wa Saudia na Imarati nchini Yemen
Kituo cha sheria cha Ain al-Insaniyah (Jicho la Ubinadamu) cha Yemen kimetoa takwimu za kushtua kuhusu maafa ya kibinadamu na kiwango cha uharibifu uliosababishwa na mashambulio ya muungano vamizi wa Saudia na Imarati katika nchi hiyo, takwimu ambazo zinaanika wazi wigo wa jinai za kivita zilizofanywa na muungano huo na waungaji mkono wake wa Magharibi…
Onyo kali la Yemen kwa muungano wa Saudia kuhusu kuendelea kuporwa nishati ya nchi hiyo
Huku uporaji wa mafuta ya Yemen ukiwa unaendelea, Abdul Aziz bin Habtour, Waziri Mkuu wa Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen ametahadharisha kuwa, iwapo uporaji huo utaendelea, Wayemen watalazimika kuzilenga meli za mafuta za muungano wa Saudia. Vikosi vya jeshi la Yemen siku ya Jumatatu viliilazimisha meli ya mafuta iliyokuwa inapanga kukaribia bandari ya…
Yemen: Zaidi ya watoto elfu 4 wa Yemen wameuawa katika mashambulizi ya muungano wa Saudia
Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen imetangaza kuwa zaidi ya watoto elfu 4 wa Yemen wameuawa tangu kuanza kwa mashambulizi ya muungano vamizi unaoongozwa Saudi Arabia. Shirika la kisheria linalofuatilia matukio yanayohusiana na watoto wa Yemen limetangaza katika ripoti yake kuwa watoto elfu 4 na 17 wameuawa na wengine 4,588 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya…
Abdulsalam: Baadhi ya makundi ya Wayemen yanafaidika na kuendelea umwagaji damu
Mkuu wa ujumbe wa serikali ya uwokovu wa kitaifa ya Yemen katika mazungumzo ya amani ya nchi hiyo ameeleza kuwa, baadhi ya mirengo ya ndani huko Yemen yenye mfungamano na Riyadh yamegeuka na kuwa wafaidikaji katika vita huko Yemen. Saudi Arabia huku ikiungwa mkono na Marekani, Imarati na nchi nyingine kadhaa mwezi Machi mwaka 2015…
Idadi ya watoto waliouawa vitani nchini Yemen yapindukia 8,000
Taasisi moja ya masuala ya sheria imetangaza kuwa, idadi ya watoto waliofanywa wahanga wa vita vya muungano vamizi wa kijeshi wa Saudia dhidi ya Yemen imeshapindukia elfu 8. Shirika la habari la Mehr limeinukuu televisheni ya al Mayadeen ikiripoti habari hiyo iliyotangazwa na taasisi ya kisheria ya “Intisaf” na kuongeza kuwa, kuna uwezekano mkubwa idadi…
Zaidi ya watoto wachanga 80 wanafariki kila siku mara baada ya kuzaliwa nchini Yemen
Afisa wa Wizara ya Afya ya Serikali ya Kitaifa ya Wokovu ya Yemen amesema zaidi ya watoto wachanga 80 hufa kila siku kutokana na ukosefu wa vifaa vya matibabu. Tangu kuanza kwa vita dhidi ya Yemen mwezi Machi 2015, muungano wa Saudia umeiwekea nchi hiyo mzingiro wa kila upande. Uhaba mkubwa wa fueli nchini Yemen…
Yemen yalaani mauaji ya kijana Ali Atef huko Riyadh
Wizara ya Masuala ya Wageni ya Yemen imelaani mauaji yaliyofanywa na vyombo vya usalama vya Saudia dhidi ya raia wa nchi hiyo”Ali Atef Hazban Al-Ali” mjini Riyadh huku familia yake ikifichua maelezo ya kushtua ya tukio hilo. Mtandao wa Al-Alam umeripoti kuwa, familia ya “Ali Atef Hazban Al-Ali” imethibitisha katika mkutano na waandishi wa habari…