
Tanzania, Zambia zakubaliana kurejesha uhusiano
Dar es Salaam. Tanzania na Zambia zimekubaliana kurejesha uhusiano wao ambao miaka ya karibuni ulilegalega, huku viongozi wa mataifa hayo wakikubaliana kuimarisha uhusiano wa kisiasa na kuwaunganisha watu. Rais wa Zambia Haikendi Hichilema amefanya ziara nchini ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu kuingia madarakani ambapo alifanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan….

Zambia kujenga bomba la dizeli kutoka Tanzania
Zambia imeanza kujenga bomba lenye urefu wa kilomita 700 (maili 435) ili kuingiza mafuta ya dizeli kutoka nchi jirani ya Tanzania ambapo uwekezaji wa awali wa mradi huo ni dola milioni 300. Waziri wa Nishati wa Zambia Peter Kapala alisema Jumapili kwamba bomba hilo jipya litaenda sambamba na la sasa lakini litakuwa la kisasa zaidi….