Tanzania, Kenya zakubali kusuluhisha mzozo wa usafiri wa anga katika kipindi cha siku tatu

Tanzania na Kenya zimekubaliana kutatua vikwazo vya usafiri wa anga kati ya nchi hizo mbili ndani ya siku tatu zijazo, Hayo yalisema jana Jumatatu na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, January Makamba.

Makamba amesema kuwa, amefanya mazungumzo na Musalia Mudavadi, Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri wa Kenya na Waziri wa Mambo ya Nje na Masuala ya Diaspora na kufikia makubaliano ya pande zote kuwa vikwazo vilivyowekwa vya usafiri wa anga kati ya nchi hizo mbili.

Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa X, January Makamba amesema: “Pamoja na mamlaka husika, tumeazimia kusuluhisha suala hili ndani ya siku tatu kwa kutegemea makubaliano yaliyopo.”

Mapema jana Jumatatu, mamlaka ya usafiri wa anga ya Tanzania ilitangaza kusitishwa safari zote za ndege za shirika la ndege la Kenya Airways zinazounganisha mji mkuu wa Kenya, Nairobi, na kitovu cha kibiashara cha Tanzania, Dar es Salaam. Hatua hiyo ilikuwa imepanga kuanza kutekelezwa kuanzia tarehe 22 mwezi huu wa Januari, 2024.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ilieleza katika taarifa yake kwamba uamuzi wao ni jibu la hatua ya hivi karibuni ya Kenya ya kukataa ombi la Tanzania la kuruhusu shirika lake la ndege, Air Tanzania Company Limited kufanya safari za mizigo kati ya Nairobi na nchi nyingine.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotiwa saini na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza Johari, Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ilitaja hatua ya Kenya ya kuikatalia Tanzania kutuma ndege zake za miziko huo Nairobi hadi nchi ya tatu kuwa ni ukiukaji wa Kifungu cha 4 cha makubaliano ya Huduma za Ndege yaliyotiwa saini kati ya nchi hizo mbili mwaka 2016.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *