Tanzania Kutumia Jeshi la Urusi Kuwaokoa Wanafunzi Waliokwama Ukraine

Wanafunzi hao waliokuwa wanasomea katika Chuo Kikuu cha Sumy nchini Ukraine, watahamishwa hadi eneo salama nchini Urusi ili kuepuka vita.Wanafunzi hao watapokelewa na jeshi la Urusi kwenye mpaka wa taifa hilo.

Hatua hiyo ni kufuatia mazungumzo ya kidiplomasia kufanyika kati ya serikali ya Urusi na Tanzania kuridhia.

Tanzania imetangaza kuwa Urusi itawasadia wanafunzi Watanzania waliokwama Ukraine kuondoka nchini humo iliyovamiwa na Urusi ili kusafirishwa hadi eneo salama.

Wanafunzi hao waliokuwa wanasomea katika Chuo Kikuu cha Sumy nchini Ukraine, watahamishwa hadi eneo salama nchini Urusi ili kuepuka vita wakisubiri kurejeshwa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi mnamo Jumamosi Machi 5, wanafunzi hao waliagizwa kuelekea eneo la Sudja ambako watapokelewa na jeshi la Urusi.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *