Tanzania yaruhusiwa kusafirisha mahujaji 11,000

Dar es Salaam. Wakati nchi ya Saudi Arabia ikiruhusu mahujaji milioni moja kote duniani kwenda kuhiji kwa mwaka huu,Tanzania imeruhusiwa kupeleka mahujaji 11,000.

Hayo yamesemwa leo Jumamosi Juni 25,2022 na Mkurugenzi wa Hijja, Alhaji Haidari Kambwili, kwenye semina ya wanaojindaa na safari ya kwenda kuhiji,  iliyofanyika ofisi za makao makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) Kinondoni  jijini Dar es Salaam.

Alhaji Kambwili amesema idadi hiyo itawahusu Watanzania kutoka Bara na Visiwani  licha ya kuwa mpaka sasa waliothibitisha kwenda ni 2700 tu.

“Kutokana na janga la Uviko 19 Saudia wametoa idadi ya watu watakoruhusiwa kwenda  Hijja mwaka huu kuwa ni milioni moja na sisi ndio hivyo tumepewa nafasi ya watu 11,000,”amesema.

Hata hivyo, amesema kwa kuwa bado hawajafikia idadi iliyotolewa na kwamba nafasi kwa anayetaka kwenda  zipo hadi siku mbili kabla ya safari inayotarajiwa kuwa Julai 3, 2022.

Wakati kuhusu gharama za kwa anayetaka kwenda alisema ni dola za Marekani 6,600 ambayo ni sawa na wastani wa  Sh16 milioni. Fedha hizo zitahusisha usafiri wa kwenda na kurudi, malazi, chakula na matibabu kwa njia ya bima ya nchini Saudi Arabia.

Kwa wale ambao walishindwa kusafiri mwaka 2019 na walikuwa tayari wameshalipia baada ya safari hiyo kusitishwa kutokana na mlipuko wa Covid, wao watatakiwa waongeze dola 2000 kutoka dola 4500 walizolipa awali,”alifafanua Alhaji Kambwili.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *