Duru za Misri zimefichua kuwa, utawala wa Kizayuni ulituma ujumbe wa usalama mjini Cairo kwa hofu ya kutokea mlipuko kwa mnasaba wa matukio yajayo ya Palestina.
Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Fars News Agency, duru za Misri zimesema kuwa, ujumbe wa usalama wa Kizayuni hivi karibuni ulisafiri hadi Cairo na kukutana na maafisa wa kijasusi wa Misri.
Kwa mujibu wa Sama, ujumbe huo ulijadiliana na maafisa wa kijasusi wa Misri kesi kadhaa ambazo zina changamoto kubwa kwa utawala wa Kizayuni na kuathiri usitishaji vita kati ya utawala huo na makundi ya Palestina.
Safari hiyo inakuja wiki chache tu kabla ya matukio yanayoweza kuzusha tena mapigano kati ya Wapalestina na utawala wa Kizayuni, ripoti hiyo imesema. Tel Aviv inahofia operesheni ya Wapalestina Siku ya Dunia (Machi 30) mbali na matukio mengine, kama vile kumbukumbu ya maandamano ya kurejea mwezi Aprili, kumbukumbu ya vita vya Seif al-Quds mwezi Mei, siku ya Nakba Mei 15, na siku ya utekaji nyara wa Palestina mnamo Aprili 17.
Duru hizo zimeongeza kuwa, vikosi vya usalama vya utawala huo ghasibu wa Kizayuni vinahofia hali ya kulipuka au kufanya maandamano katika matukio tajwa kwa njia ambayo inaweza kusababisha mapigano hususan kwa vile hali ya usalama katika ardhi zinazokaliwa kimabavu za mwaka 1948 pia imekuwa nyeti.
ripoti ilisema ilieleza kua ujumbe wa Israel pia ulijadili upatanishi mpya wa Misri na mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Hamas ili kukubaliana juu ya hatua za usalama wakati wa Ramadhani katika mji wa Jerusalem na eneo la Bab al-Amoud huko Jerusalem.
Katika mahojiano na Al-Mayadin jana usiku (Jumatatu usiku), mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, Saleh al-Arouri, alisisitiza kwamba uvamizi wowote wa Israel dhidi ya waumini katika Msikiti wa Al-Aqsa utazidisha hali ya wasiwasi. Hivi leo utawala wa kibeberu unakabiliwa na mtihani wa Quds na Msikiti wa Al-Aqswa, na umefika wakati wa wao kujua kwamba Quds na maeneo matukufu na Msikiti wa Aqswa ni mstari mwekundu kwetu.
Amesisitiza kuwa: Utawala wa Kizayuni utafungua milango ya moto wa Jahannamu kwa kuwazuia waumini kuingia katika Msikiti wa Al-Aqsa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.