Tel Aviv inahofia jeshi la Yemen huenda likavamia maeneo yanayomilikiwa kimabavu

Vyanzo vya Habari kwa lugha ya Kiebrania viliripoti kuwa Tel Aviv inachunguza shambulio la jeshi la Yemen dhidi ya Abu Dhabi kwa kuhofia mashambulizi kama hayo katika maeneo yaliyokaliwa na kumilikiwa kimabavu.

Jana (Jumanne) Idhaa ya Kiebrania ya Kan iliripoti kwamba Tel Aviv ilikuwa ikichunguza ripoti za shambulio la ndege isiyo na rubani ya Sanaa dhidi ya Abu Dhabi kutokana na hofu ya kutokea shambulio kama hilo dhidi ya Palestina inayokaliwa kimabavu.

“Mojawapo ya hali ambayo Israel inahofia ni shambulio la ndege zisizo na rubani na makombora yaliyorushwa kutoka Yemen,” tovuti ya habari ya Arab 48 ilimnukuu Kahn akisema. Umbali kati ya Yemen na Abu Dhabi ni sawa na umbali kati ya Yemen na mji wa Eilat iliyopo kusini mwa Israel. “Shambulio hili linaonyesha uwezo wa hali ya juu wa Houthis.”

Hapo jana baada ya Sanaa kutoa onyo kwa mara kadhaa kwa Abu Dhabi kuhusu kuingilia kwao masuala ya ndani ya Yemen na kupelekea kuongezeka kwa mivutano nchini humo, vyombo vya habari vya Imarati viliripoti kuwa baadhi ya maeneo ya nchi hiyo yalilengwa na ndege zisizo na rubani.

“Mohammad al-Bukheiti,” mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya vuguvugu la Ansarullah la Yemen aliiambia Al-Arabi kabla ya shambulio hilo: “Kuna makubaliano kati ya Saudi Arabia na UAE, ya kwamba Saudi Arabia itaikabidhi UAE majimbo yote yaliyopo kusini mwa Yemen ikiwemo Shabwa, na ikawa kwamba UAE itatumia uwezo wake wote wa kijeshi kama ujira au malipo kwa Saudia kama ilivuokua zamani. [nchini Yemen].”

Al-Bukheiti alionya kua: “Kwa hatua tuliyofikia tunaishauri UAE ya kua isiendelee na hatua zenye kulenga mvutano, kwa sababu mvutano huu ukiendelea, Yemen italazimika kushambulia ndani kabisa ya ardhi yake. “Tupo tayari kivita”.

Kufuatia onyo hilo, vyanzo vya habari viliripoti siku ya Jumatatu, tarehe 17 Januari ya kwamba meli tatu za mafuta zililipuka na kushika moto katika eneo la Al-Masfah lipatikanalo UAE na kisha baada ya hapo kukatolewa ripoti ya moto. Al-Masfah ni eneo lenye viwanda lililopo kusini magharibi mwa Abu Dhabi ya UAE.

Saa chache baadaye, msemaji wa Jeshi la Yemen Brigedia Jenerali Yahya Sarei alitangaza rasmi kwamba vikosi vya Yemen vimevishambulia viwanja vya ndege vya Dubai na Abu Dhabi kwa makombora na ndege zisizo na rubani.

Kufuatia shambulio hilo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Yair Lapid jana aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter: “Ninalaani vikali shambulizi la leo la ndege zisizo na rubani lililotokea mjini Abu Dhabi na natoa rambirambi zangu kwa familia za wahasiriwa na kuwatakia majeruhi ahueni ya haraka. Israeli iko Pamoja na UAE.

Kabla ya hapo, tovuti ya habari ya Vala iliripoti kuhusu uwezo wa ndege zisizo na rubani za jeshi la Yemen na kamati maarufu ya kwamba shambulio la ndege zisizo na rubani za jeshi la Yemen na kamati maarufu zimeathiri vituo vya kistratijia vya Saudi Arabia, Tel Aviv na Magharibi.

Vala iliripoti kuwa shambulio la ndege zisizo na rubani lililotekelezwa na jeshi la Yemen na kamati maarufu mnamo 2019 dhidi ya kampuni ya Saudi ijulikanayo kama Aramco “wakati huo” liilishtua Israeli na Magharibi.

Kambi hiyo ya lugha ya Kiebrania imeongeza kuwa, ubora uliopo kwenye ndege hizo zisizo na rubani zilizotumika katika shambulizi hilo na namna Aramco ilivyolengwa kumezishangaza idara za kijasusi za Israeli na nchi za Magharibi na ikawa kwao kama nukta ya  kchukua tahadhari.

Tovuti hiyo ilirejelea haswa shambulio la UAV kwenye Aramco mnamo Septemba 14, 2019.

Kulingana na jeshi la Yemen na kamati za wananchi, ndege 17 zilitumiwa katika shambulio la 2019 katika kampuni ya Saudi ya Aramco katika maeneo ya Baqiq na Kharis iliyopo mashariki mwa Saudi Arabia, ambayo ilisababisha moto mkubwa katika sehemu pana yenye vituo viwili vya kusafisha mafuta vya Aramco. kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia, kituo hicho kilifungwa hadi ukarabati hadi ukarabati utakapofanyika.

 

 

 

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *