Trump atalipa gharama kubwa kwa mauaji ya Soleimani na Muhandis: Makundi ya mapambano ya Iraq

Kiongozi wa kundi la mapambano la Asa’ib Ahl al-Haq la nchini Iraq amesema rais wa zamani wa Marekani Donald Trump atalipa gharama kubwa kwa kuhusika na mauaji ya kigaidi dhidi ya mashujaa wawili wa mapambano dhidi ya ugaidi, Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Muhandis.

Qais al-Khazali aliyasema hayo hivi karibuni katika hafla ya kuwakumbuka makamanda hao wawili wanaoheshimika na wenzao kadhaa katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad.

“Tunatangaza utiifu wetu kamili kwamba hakika tutalipiza kisasi kwa damu ya makamanda na mashahidi wetu walioanguka. Hatutaogopa kusema ukweli. Ni wakati muafaka wa sisi kujua kikamilifu kuhusu mazingira yaliyozunguka mauaji hayo. ” Amesema Khazali.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Kitengo cha Uhamasishaji cha Iraqi (PMU) pia amesema maadui walifanya makosa makubwa ya kumuua Jenerali Soleimani, na kwamba mazishi yake nakubwa yalionyesha wazi umaarufu mkubwa aliokuwanao katika eneo.

“Ushiriki wa mamilioni ya watu katika mazishi ya Jenerali Soleimani ulidhihirisha wazi kuwa ana hadhi ya juu katika mioyo ya watu. Ingawa Donald Trump alipanga uhalifu wa mauaji yake, lakini haikuchukua muda mrefu kabla ya rais huyo wa zamani wa Marekani kutupwa kwenye jalala la historia.” Amesema Falih al-Fayyadh.

Jenerali Soleimani, kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC), Abu Mahdi al-Muhandis, Naibu Mkuu wa kitengo cha PMU, na wasaidizi wao waliuawa kinyama katika shambulio la ndege zisizo na rubani za Marekani zilizoidhinishwa na Trump karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad mnamo Januari 3, 2020.

Siku mbili baada ya shambulio hilo, wabunge wa Iraq waliidhinisha mswada ulioitaka serikali kuvifukuza vikosi vyote vya kijeshi vya kigeni vinavyoongozwa na Marekani nchini humo.

Mashujaa wawili hao wa kupambana na ugaidi waliheshimika sana katika eneo la Mashariki ya Kati kutokana na nafasi yao muhimu katika kupambana na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh katika eneo hususan katika nchi za Iraq na Syria.

Mnamo Januari 8, 2020, IRGC ililenga kambi ya Ain al-Asad ya Marekani katika mkoa wa Anbar magharibi mwa Iraq kwa wimbi kali la makombora ikiwa ni katika sehemu ya kulipiza kisasi cha mauaji ya Luteni Jenerali Soleimani.

Iran imelitaja shambulio hilo la makombora dhidi ya kambi ya Ain al-Assad kama “kofi la kwanza.”

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *