Rais huyo wa zamani wa Marekani alikosoa sera za utawala wa Biden dhidi ya Iran.
Rais mstaafu wa Marekani, Bw. Donald Trump, amekuwa akimkosoa Rais Joe Biden hivi majuzi huku akizikosoa sera zake kuhusu Iran kulingana na taarifa za hivi punde.
Kwa mujibu wa ripoti ya Newsmax, Trump alidai katika hotuba yake kwamba serikali ya Iran hivi sasa iko karibu na bomu la atomiki kuliko hapo awali; ikiwa haijamiliki hadi kufikia sasa !
Matamshi ya Trump kuhusu kuimarishwa kwa nchi Iran yamekuja katika wakati ambapo yeye kwa kujitoa katika JCPOA na kuzipa kisogo ahadi za Washington na kuwatishia Wazungu kuhusu uhusiano wowote wa kiuchumi na Iran, alisababisha kuharibika kwa makubaliano hayo na kusababisha kuimaika kwa nchi ya Iran zaidi kuliko kiasi kilichokua kimeainishwa katika JCPOA.
Hata hivyo Iran imekuwa ikisisitiza mara kwa mara kuwa silaha za nyuklia hazina nafasi katika stratijia ya kijeshi na ya kiulinzi ya nchi hiyo, na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki unathibitisha shughuli za Iran.
Katika hotuba yake kwa wahafidhina mjini Tampa, Florida, Trump alidai: “Soma ripoti hizo. Wana urutubisho wanaohitaji.” Na wanaweza kuwa na silaha za nyuklia katika kipindi kifupi sana. Ninazungumza juu ya miezi michache au chini na wanaweza kuwa na moja tayari …
Akirejelea madai haya, Trump alionya kwamba Iran ya nyuklia itabadilisha ulimwengu vibaya zaidi kuliko kile ambacho Wademokrat wenye msimamo mkali wamefanya kwa ajili ya kuiangamiza nchi yetu.
Katika sehemu ya hotuba yake, Trump pia alisema kuwa Marekani iko katika matatizo makubwa ya kutuma misaada ya kifedha na silaha kwa Waukreni katika vita na Urusi.
Wakati wa hotuba yake mjini Florida, rais huyo wa zamani wa Marekani alikumbuka kwamba aliziomba NATO na nchi zilizo nz uwanachama wa Umoja wa Ulaya kuongeza bajeti yao ya kijeshi hadi 2% ya Pato lao la Taifa.
Trump alisema, wakati huo, Ulaya ilikuwa ikiitumia vibaya na kuinyonya Marekani, na sasa Ukraine inaifanyia nchi yake vivyo hivyo.
Alisema zaidi: Tumetoa zaidi ya dola bilioni 60 kwa Ukraine. Naam, nchi za Ulaya zimeathirika zaidi na vita hivi kuliko sisi, lakini wamelipa sehemu ndogo ya kiasi hiki.