TUSIJE TUKASAHAU: Vijana Waliojisajili Kidijitali Kwa Mpango Wa Kazi Mtaani Hawajaanza Kazi

MNAMO Oktoba 20, 2021 Rais Uhuru Kenyatta aliamuru Hazina ya Kitaifa kutenga Sh10 billion za kufadhili awamu ya tatu ya Mpango wa Kazi Mtaani.

“Naamuru Hazina ya Kitaifa kutoa Sh10 bilioni za kugharamia awamu ya tatu ya Mpango wa Kazi Mtaani. Mpango huo ambao unalenga kufaidi zaidi ya vijana 200,000 utatekelezwa katika kaunti zote 47 nchini huku maeneo yenye watu wengi yakitengewa nafasi zaidi,” Rais Kenyatta alisema alipoongoza sherehe za kitaifa za Mashujaa Dei katika uwanja wa Wang’uru, kaunti ya Kirinyaga.

Baada ya hapo Katibu katika Wizara ya Uchukuzi anayesimamia Idara ya Nyumba na Ustawi wa Miji Charles Hinga alizindua shughuli ya usajili wa vijana kidijitali kwa mpango huo.

Serikali isije ikasahau kuwa miezi mitano baada ya Rais Kenyatta kuamuru pesa za kufadhili mpango huo zitolewe, vijana waliojisajili hawajaanza kazi.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *