Ubalozi wa Palestina Tehran walaani uhasama wa Uingereza dhidi ya Hamas

Faraan: Taarifa hiyo imesema badala ya uhasama huo serikali ya Uingereza inapaswa kutambua rasmi uhuru wa Palestina.

Aidha Ubalozi wa Palestina mjini Tehran umesema nchi ambazo zinatambua taifa la Palestina ni zaidi ya nchi ambazo zimeutambua utawala wa Kizayuni wa Israel. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Uingereza ndio chanzo cha matatizo ya taifa la Palestina kwa muda wa miaka 73 sasa.

Ikumbukwe kuwa, katika kuendeleza siasa zake dhidi ya taifa la Palestina na kuunga mkono utawala haramu wa Israel, Uingereza imetuhumu na kuitangaza Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Paletina Hamas kuwa ni kundi la kigaidi.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *