Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
(Principal Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)
Delivered at: Masjid Baitul ul Ateeq
Lahore – Pakistan
Hotuba ya Ijumaa – 12 April, 2024
Hotuba ya 1 :Taqwa na Tawakkul hutoa dhamana ya ulinzi
Hotuba ya 2: Udhalili wa Waislamu kwa sasa unaweza kuondolewa na toba ya kivitendo
Bila ya kuwa na Taqwa maisha yanakuwa yameharibika hapa duniani na kesho akhera. Kiuhalisia mwanadamu hujiangamiza mwenyewe hapa dunia na kisha kuendelea hadi Akhera. Mfano wa maisha haya na Akhera mfano umekwisha elezwa ndani ya hadithi ya kwamba dunia ni shamba la akhera ambapo mwanadamu hupanda mazao yake katika shamba hili ambalo ni dunia. Chochote atakacho kipanda ndicho atakuja kuvuna mwisho wa siku na hakuna kitu ambacho kitatoka nje ya hapa. Chochote unacholima ndicho utakacho kivuna. kwa mkulima anapokuwa kapanda mbegu shambani anatakiwa kulinda shamba hili. Anatakiwa kulimwagilia shamba, kulilinda kutokana na wanyama na wadudu. Hivyo basi kupanda mbegu ni hatua moja na umuhimu huo pia upo kwenye kulinda. Hivyo basi Mwenyezi Mungu alitengeneza mfumo wa uongofu ndani ya mwanadamu na kisha Taqwa ndio imewekwa kuwa kama mlinzi wa kulinda shamba hili la uongofu ambapo mkulima pia anapaswa kufanya hivyo mwenyewe. tunaweza kuona baadhi ya nyakati kwamba watu waliosoma elimu ya dini, Fiqh, Hadith na maadili lakini pamoja na haya yote hawapati Taqwa. Hivyo basi hawa watakuwa wamelima bila ya kupalilia. Sasahivi kwao elimu ya akhera sio katika elimu zao isipokuwa majaribio ya maisha ambayo wamekuwa wakiyaishi bila ya Taqwa. Tunakuwa ni wenye kuvutiwa na dini, tunasoma sheria na tunajifunza kutenda baadhi ya matendo lakini hatuyalindi. Hivyo basi, kila tunacho kipanda tunakivunja wenyewe pia.
Mfano mwingine unaotolewa na Qur’an ni kuhusu mwanamke ambaye hufuma kapeti mchana na kisha kuifumua usiku yeye mwenyewe. Qur’an inasema usipotweza matendo yako kama hivi. hii ni Habtul ‘Amal, ambapo mtu hufanya matendo mazuri kisha huyafuta hayo mazuri yote. Ni kama mtu ambaye mfuko wake una tundu. Mtu inabidi alinde matendo yake la sivyo yatapotea. Taqwa haiji kwa kuipata elimu kwa kufanya baadhi ya ibada . kwa ajili ya ulinzi mtu anapaswa kuwa na mipango na usimamizi wa kulinda kila Nyanja ya maisha na Allah amekwisha lieleza hili. Kama ulivyokuwa na njia nyingi za kulinda vitu nyumbani kwako, hivyo kila kitu kina namna ya kukilinda. Hivyo aina moja ya Taqwa haiwezi kuweka ulinzi kwenye kila kipengele cha maisha. Taqwa kwa wafanya biashara ni ya mfumo tofauti, kwa wakulima, wanawake na mahusiano haya yote yana mifumo tofauti ya Taqwa. Allah ametaja nyanja zote hizo za maisha ambapo ni muhimu sana kuwa na uchamungu.
Uwanja mmoja ni Jihadi. Surah Maida, Aya ya 11
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ هَمَّ قَوْمٌ أَنْ يَبْسُطُوا إِلَيْكُمْ أَيْدِيَهُمْ فَكَفَّ أَيْدِيَهُمْ عَنْكُمْ ۖ وَاتَّقُوا اللَّهَ ۚ وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ {11}
Enyi mlioamini! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yenu, walipotaka watu kukunyoosheeni mikono, naye akizulia mikono yao kukufikieni. Na mcheni Mwenyeji Mungu . na waumini wamtegemee Mungu tu.
Ujumbe unawahutubia waumini ya kwamba kwanza wakumbuke na wavutiwe na neema ambazo Mwenyezi Mungu kuwaneemesha kwazo. Na neema hii ni pindi mlipokuwa mmezingirwa na maadui na walikuwa karibu yenu na wangeli kumalizeni na kukusambaratisha nyote. Kisha Allah akazuia mapanga yao, mashambulizi yao na mikono yao isiwafikie. Na hamkuwa mnalifahamu hili, lilifanywa na Allah. Hivyo basi kuwa na Taqwa na waumini ndio tu wenye kumtegemea Allah.
Allah amekuokoeni na mashambulizi haya lakini mnapaswa kuwa na ulinzi na mfumo wa kujilinda endelevu siku zote. Sio kwamba kwa kua Allah kawalinda basi mnatakiwa kubaki bila ya kufanya chochote. Baadhi ya watu wanaishi katika hofu mwaka mzima kwamba wapo kwenye kuwindwa na maadui. Lakini baadhi yao hawafanyi lolote ambapo hutengeneza maadui au maadui huwaendea na kiuhalisia maadui huwapenda watu wa namna hii. Kuna watu wengi ambao hujifanya kuwa ni waumini lakini kumbe ni madai tu. Kili mmoja leo hudai kwamba ni waumini lakini je Allah ameshawapa majaribu juu ya Imani zao?. Hawa sio waumini lakini wanajaribu kumhadaa Allah na watu wengine lakini hawadanganyi ila nafsi zao wenyewe. Aina hii ya waumini ni marafiki wakubwa wa maadui. Kama tutachukua matukio yanayojiri sasa, tutapata kwamba hawa ni wabaya zaidi ya maadui. Hali ambayo ipo Gaza, Palestina na unaona hali waliyo nayo Waislamu ulimwenguni. Ni mbaya zaidi ya makafiri. Na juu ya waumini kuna maulama tunaweza kuona tabia zao kuelekea Gaza. Hilo ni baya zaidi ya maadui na Wazayuni. Allah anasema kwamba sio waumini.
Wale ambao ni waumini wapo kwenye hatari kabisa. Maadui wana hasira nao sana kwa sababu ya imani zao, kumpwekesha Allah. Tunaweza kutathmini ni akina nani ni adui zetu na kisha tutafahamu kama sisi ni waumini au hapana. Ikiwa mafasiki ni marafiki zetu na wanafurahishwa na sisi basi sisi sio waumini. Pindi inapokuwa makafiri, Washirikina, mafisadi, na Mataghuti wakawa wanafurahishwa na wewe basi ujue hakuna imani ndani yako.
Tunazingatia kutokuwa na maadui kama ni uzuri, lakini tunapaswa kununua uadui. Kama tutamuona Ibrahim, Azar ambaye alikuwa mlezi wake na Qur’an imemuelezea kama baba. Alikuwa ni mlezi wa Ibrahim. Alimwambia Azar kwamba hiki unachokifanya sio sahihi na kisha Ibrahim muda sio mrefu alimlaani Azar kwa vitendo vyake vya kumshirikisha Mwenyezi Mungu. Alisema kwamba kuna uadui baina yetu kama utaendelea kuabudu masanamu na ushirikina. Ibrahimu alimlingania kwa hatua tatu: hatua ya kwanza: Ole wako, hatua ya pili mimi sifanyi ushirikina hatua ya tatu ni mimi nina uadui na wewe. Na baada ya hapa Ibrahimu hakulala alienda kuyavunja masanamu ya kwenye hekalu. Muumini inabidi anunue uadui wa namna hii na hii ni alama ya imani. Uadui ambao walikuwa wakifanyiwa maimamu ulikuwa ni wa gharama ya kiwango cha hali ya juu. Maadui wa Imam ‘Ali (‘a) na Imam Husein (a) walipandishwa na wenyewe. Ilikuwa inawezekana kwa Imam Husein (a) kubadilisha uadui kuwa urafiki. Kama leo sisi ni marafiki wa mafisadi eti kwa sababu ni baba zetu wadogo au wajomba, shangazi na ndugu. Huu ni udanganyifu na maadui wanataka kuwaua na kuwamaliza waumini. Adui mkubwa wa Taghuti ni muumini. Imam Khomeini (r.a) aliwahutubia wasomi wasiokuwa wanasiasa mjadala wenye hoja nyepesi kwamba wale wanaosema ya kwamba maimamu hawakuwa na habari na watawala na kwamba walikuwa tu ni wenye kujishughulisha na mambo ya kiroho, je kwanini maimamu wote tunaona waliuliwa kishahidi na watawala. Sasa hawa watawala walikuwa na matatizo gani na maimamu? Kwanini Saddamu aliwaua kishahidi Shahidi Sadr na dada yake? Na wakate huo huo maulama walikuwa wameamanika na Saddam. Bali alikuwa akiwalipoa mishahara kwa sababu hawakuwa na madhara yeyote kwa maslahi ya Saddam. Lakini tukiwatazama Maimamu tunaona hawakuachwa waishi kwa amani na wote waliuawa ima kwa upanga au kwa sumu. Imam Khomeini (r.a) aliwauliza maulama kwanini Maimam waliuliwa kishahidi? Hii ina maana kwamba watawala na mataghuti walikuwa na matatizo na Maimam. Maimam walikuwa viongozi wenye harakati na ndio maana watawala walikuwa wanawaogopa. Ni kama ilivyokuwa kwa Maimam mataghuti ni maadui wa waumini pia na watafanya mambo yote ya mipango ya siri, mateso na tuhuma ili kuwapata waumini au kushambulia shakhsiya zao na kuwatoa kwenye njia yao.
Kwa kuteremshwa hii Aya kuna mambo mengi sana nyuma yake yametajwa. Wengi wanasema ya kwamba Mtume ( s.a.w) alikuwa amezingirwa na maadui na kisha Aya hii ikateremshwa. Lakini kwa namna anavyosema ‘Allama Tabatabai ni kwamba Aya haina kiashiria chochote kinacho ashiria ya kwamba ni Mtume (s.a.w) aliyekuwa kazingirwa. Aya inazungumza kwa ujumla na ikizungumza na waumini wote ambao walikuwa pamoja na Mtume. Na hakuna ushahidi sahihi ambao unathibitisha hili lilikuwa ni tukio gani. Mna mtirirko wa sauti wa Aya pia hauashirii kama kulikuwa na tukio maalumu bali inazungumzia kwa ujumla. Tunaweza kusema ya kuwa hali ilikuwa hivi katika vita vyote. Hivyo sera ya jumla imewasilishwa na Qur’an. Kila jamii ilipo azimia kuwamaliza waumini basi Allah aliiondoa hatari. Na sasa waumini wanatakiwa kuupata uchamungu na kumtegemea Allah.
Kama utakuwa na uchamungu basi Allah atakulinda . kama tutafikiri kwa kina tunaona kwamba msingi wa sera ya Qur’an umetajwa hapa katika Aya hii. Taqwa na Tawakkul ndio dhamana ya kubaki salama kutokana na maadui. Hili linawezekana pale ambapo Taqwa itakuwa sio kanuni ya kimaadili bali ni kanuni ya Qur’an na mfumo. Taqwa na Tawakkul ni mifumo miwili kutoka kwa Allah. Waumini wanaweza kupitia kipindi cha vitisho na hatari kutoka kwa maadui kwa sababu ni sharti la njia ya imani. Ni kama kwa Imam Husein ( a) kila rafiki yake, ndugu yake na wengine walikuja kwake kwa kumuonea huruma na wakijaribu kumsimamisha na ili aachane na kusimama kufanya mapambano dhidi ya utawala. Abdullah bin Umar ambaye alikuwa ni shakhsiya ya kuheshimika alikuja kumzuia Imam Husein (a) pia asiende vitani. Alikuwa ni mtu mwenye kujishughulisha zaidi na ibada mbali mbali. Alimsisitiza sana Imam Husein (a) kwamba asiendelee na harakati yake. Imam Husein ( a) alimuuliza: niambie je njia niliyo ichukua ni ya makosa? Abdullah alijibu hapana sio ya makosa na hujakosea lakini upo kwenye hatari na sisi tunataka tukulinde na hatari. Imam (a) alisema kama ninataka kujikinga na hatari na vitisho basi inabidi nifanye makosa. Muumini anaweza kuondoa hatari kwa kufanya kosa lakini Allah anasema hutakiwi kufanya kosa bali chukua vitisho badala yake.
Huwezi kukubaliana na maadui na Allah haruhusu. Pindi mwenyezi Mungu alipowaweka waumini chini ya vitisho alitengeneza mfumo kwa ajili ya ulinzi. Allah aliweka mpangilio na kila mpangilio alio uweka Allah ameutengeneza kupitia mfumo. Kwa kupitia mfumo sheria huwekwa sheria na chochote unachotaka kukifanya kitatimia pale tu utakapo kihusisha na mfumo. Ukiwa utaukiuka mfumo na kuukwepa kazi yako haitatekelezeka kwa ukamilifu. Sio kwamba Allah jana usiku alishindwa kuamua kukupa kitu na asubuhi ndio akaamua kukupa thawabu. Hili haliwezekani kwa sababu hili lengo la pili linafungamana na kitu ambacho hakikuwepo huko na sasahivi kimetokea. Ni kitu ambacho hakikuwa katika malengo ya Allah na kisha Allah akakifanya. Hivyo basi ni kwa namna gani tutaomba dua zetu na kukubaliwa? Je ni kwa kuwa tulilia sana na Allah akaamua kutupa? Kwa hiyo Dua zetu zinaenda wapi? Maombi haya hayaendi ofisi yeyote, huenda ndani ya mfumo. Ulimwengu imeundwa kwa mfumo. Kwa namna yeyote utakayotaka kuweka ndani ya mfumo na mfumo utatambua kama ni la kimfumo au hapana. Ni kama katika programu yako ukitaka kuingiza kitu ikawa haikubali. Chochote unachoingiza ndani ya mfumo na unapata kila kitu kutoka kwenye mfumo. Kwanza unaingia ndani ya mfumo.
Katika Aya hii kuna mifumo miwili na kanuni za kimatendo za kimaisha ambazo ni Taqwa na Tawakkul. Maisha ya muumini hutembea juu ya reli hizi mbili kama Treni inavyo tembea juu ya reli mbili. Ikiwa utayaweka maisha yako katika reli hizi mbili basi treni itafika kwenye kituo cha mwisho. Huenda maadui watakuja njiani lakini hutakiwi kushuka yanayosalia Allah atayasimamia. Ikiwa baadhi ya kundi wakitaka kukutoa kwenye reli basi kuna mfumo mwingi wa ziada ambao yuko nao Allah na hauko kwako. Umeambiwa ukuze imani, kuwa waumini na kisha jenga safari yako ya maisha kwa Taqwa na Tawakkul. Kuna mambo mengine mengi ulimwenguni mbali na haya na kwa ajili ya haya kuna mfumo pia uliotengenezwa na Allah.
Tuliwahi kuelezea Taqwa hapo kabla na kwa sasa tunatazama nyanja za Taqwa. Taqwa katika Aya hii imeelezewa katika uwanja wa jihadi. Na kuhusu Tawakkul hii inabidi tuieleze kwani tuna picha tofauti katika akili zetu. Inabidi tuone ni upi uhalisia wa Tawakkul kama ulivyo wasilishwa na Qur’an.
Hotuba ya 2
Mwezi wa Ramadhan ulikuwa ni fursa adhimu ya kupata Taqwa. Wale waumini ambao waliitumia Ramadhani yao kama tulivyo elekezwa kutoka katika miongozo ya Ahlul Bayt ( a) walipata taufiki ya kuabudu na kwa sasa tumekuja katika njia ya Taqwa hivyo wanatakiwa kuielezea Taqwa.
Kama ilivyotajwa ndani ya hotuba ya kwanza kuhusiana na Aya ya 11 ya Suratul Maida. Ndani ya Aya hii Allah humfanya muumini akumbuke wakati maadui walipotaka kukumaliza na Allah aka kulindeni kwa kuidhibiti mikono ya maadui. Hii ni sera ya Qur’an kwamba waumini wakipata Taqwa Allah huwazuia. Lakini leo hii haitokei ambapo mikono ya madhalimu wote inawasogelea waumini na kutaka kuwaangamiza.
Kama ilivyo jadiliwa katika mwezi wa Ramadhani katika hotuba za Qur’an., tulijadili kuhusu Aya ya50 YA Suratul Baqarah ambapo Allah anawafanya wakumbuke neema ambapo Allah aliwaokoa kutoka kwa Fir’aun. Bani Israel walikuwa wakiishi katika ardhi ya Kanan ambayo ni Palestina, Syria, Lebanon na Jordan. Kutokana na matatizo ya kiuchumi walihamia Misri na vizazi vyao vikakua huko kwa mamia ya miaka. Walikuwa wakiheshimiwa kwa kuwa walikuwa watoto wa mitume lakini taratibu taratibu walikuja kuwa watumwa wa Misri na wakaingia katika adhabu kali kutoka kwa Bani Israel. Ili kuwaokoa Allah alimfanya Musa azaliwe. Nukta ya msingi hapa ipo kwenye vitu viwili ambavyo viliwafanya wafeli. Kitu cha kwanza ilikuwa ni udhaifu uliokuwa ndani ya Bani Israel ambao ni maadili, utu na jamii. Na kitu cha pili ilikuwa ni mfumo wa utawala wa Fir’aun ambao ndio ulikuwa chanzo cha utumwa wao. Mambo haya mawili siku zote yapo. Allah anasema kama utapata Taqwa na kufanya Tawakkul basi Allah atawashinda maadui zako. Hawa masahaba wachache wa Mtume (s.a.w) wangeweza kushindwa sana na maadui lakini Allah alikuwa anawalinda kutokana na Tawakkul ambayo walikuwa wakifanya chini ya uongozi wa bwana Mtume (s.a.w).
Leo hii pia hali hii yenyewe ipo ndani ya Gaza. Kwa kipindi cha miezi sita sura kamili na ukweli wa waumini umewekwa wazi. Kwanini Allah hakuzuia mikono ya maadui? Adui baada ya kuiharibu Palestina sasahivi anapiga hatua kubwa mbele akielekea Lebanon, Syria, Iraq na Iran. Aya inasema kwamba jamii ya madhalimu imekusudia kunyoosha mbele zaidi mikono yake kukuelekeni nyinyi, maana yake walijaribu kukushambulia lakini Allah akazuia mikono yao kwa sababu mmekuwa na Taqwa na Tawakkul. Leo hii waumini wameacha Taqwa na Tawakkul ambapo adui anasogea mbele taratibu taratibu taratibu. Pindi Israel iliposhambulia Gaza Amerika na Uingereza walikuja mbele kuwasaidia. Na sasahivi wanasema kwamba ikiwa Iran itaishambulia Israel basi Amerika, Uingereza na NATO watakuja kumsaidia Israel. Tabia za waumini ni ya kutisha sana kwa sababu Israel hakuwahi kupata ujasiri, nia walio nayo leo. Imekuwa ni ngumu kumzuia Israel. Lau kama mungewazuia huko Gaza wasingefikia walipofikia leo. Leo hii waumini wanapaswa kutathmini tabia zao na kisha Allah anaweza kuzuia mikono ya maadui. Wale ambao ni watu wazima wanafahamu kwamba pindi mapinduzi yalipokuja, Wairan walikuwa ni mateka na watumwa ndani ya Iran. Bunge la Iran lilikuwa linapitisha mswada kwa stampu ya Shah ambapo hata kama mbwa wa Mmarekani angelimg’ata muiran, na muiran endapo angelimpiga mbwa basi Mmarekani alikuwa akimuadhibu muiran. Lakini ikiwa muiran atauliwa na Muamerika, basi mahakama ya Iran haina haki ya kumhukumu na kumuadhibu Mmarekani. Hii ilikuwa mbaya zaidi kuliko hata ya Fir’aun. Baada ya mapinduzi vijana walizingira ubalozi wa Amerika kwa muda wa siku mia nne. Amerika alituma kikosi maalumu ambacho kimepata mafunzo kwa ajili ya operesheni hii. Walitua Tabas katika jangwa karibu na Mashhad na kutaka kushambulia nyumba ya uongozi wa Iran. Walikuwa na mipango kamili na Wairan walikuwa hawana habari. Lakini waliposhuka katika eneo hilo na pindi wakati wa kufanya kazi yao ulipokaribia kimbunga cha vumbi kali kilikuja na Helikopta zilivyotaka kuruka zikagogana. Hivi ndivyo Allah anavyo wazuia maadui kama utakuwa na Taqwa na Tawakkul. Leo hii maadui wamenyoosha mikono yao sana lakini na vibaya zaidi lakini udhaifu ambao umeonyeshwa na Waislamu kwamba sheria za Allah haziwezi kutumika. Allah ame3tengeneza mfumo ambao unashughulikia matukio. Ikiwa mambo yanaenda kwa mujibu wa mfumo, basi mfumo utawazuia maadui. Kwa mujibu wa mfumo imani na Tawakkul ambazo waumini walitakiwa kuzionyesha hawakufanya hivyo, badala yake walionyesha uoga. Wale ambao wanaukimbia mfumo wa Allah, hawasaidiwi na badala yake wanajisalimisha kwa maadui na watawala. Ikiwa utaipata nia ya Allah bila shaka Allah atakusaidia.
Katika siku ya Eid waliwaua kishahidi vijana watatu na wajukuu watatu wa Ismael Haniya amba walikuwa Gaza. Ismael Haniya alikuwa Qatar ana alipopata habari hizi alisema damu ya watoto wangu haina thamani ya damu za Wapalestina. Leo hii nimeona picha ya mke wa Ismael Haniya akiwa kitandani Hospitali akionyesha alama ya ushindi. Halii na zaidi anaonyesha furaha kwa kuonyesha alama ya ushindi. Allah amekubali muhanga wetu huu ambao unamaanisha ushindi unakuja upo karibu nasi. Kinyume na ukuu huu tazama tabia Waislamu wengine. Wanaonekana ni wa chini kiasi gani? Ulimwengu wa Kiarabu unaonekana kuwa mchafu mbele yao. Mfumo wa Allah ni kwamba matokeo ya subira na uvumilivu vitaleta ushindi na Aqsa itakombolewa lakini udhalili wa Waislamu hautaisha. Aibu ambayo wameionyesha kwa miezi sita iliyopita itabaki na Allah atawapa dhiki sana. Kipaumbele cha Waislamu kwa sasa wanapaswa kuomba msamaha kwa Allah kwa uzembe walio ufanya na sio kwa maneno. Ni wakati ambao kila mtu anatakiwa ainuke na kila nchi ya Kiislamu inabidi waondoe ubalozi wao na taasisi zake katika nchi zote. Tunaonyesha kukosha aibu kabisa kohokana na tunavyo jionyesha. Watawala wetu wanadhani kwamba wapo salama chini ya mwamvuli wa Amerika. Hata fatwa za kuwekea vikwazo hazitolewi na wasomi wa sheria laki wanatakiwa kutoa fat’wa ya Jihadi. Lakini hili linahitaji moyo wenye ujasiri. Tunamuomba llah atutoe katika udhalili huu.