Ikiwa ni katika kuendeleza chuki na uadui wake dhidi ya Uislamu, serikali ya Ufaransa imefunga Msikiti mwingine kwa muda wa miezi sita kwa madai ya kuruhusu mawaidha yasiyokubaliwa na serikali ya Paris.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Anadolu, mkuu wa mkoa wa Bordeaux ametoa taarifa ya kuvunjwa Msikiti wa al Farouk ulioko kwenye eneo la Pessac huko Gironde, kusini mwa Ufaransa. Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa, sababu ya kufungwa Msikiti huo ni kueneza kile alichodai ni misimamo mikali ya Kiislamu.
Viongozi wa Paris wamewatuhumu viongozi wa Msikiti huo kuwa wanaruhusu mawaidha ambayo yanakwenda kinyume na sheria za Ufaransa na yanachochea mashambulio ya kigaidi.
Mkuu wa mkoa huo wa Bordeaux vile vile amedai kuwa, masheikh katika Msikiti huo wanatoa mawaidha yanayousema vibaya utawala wa Kizayuni wa Israel na pia kuunga mkono taasisi na watu aliodai wana misimamo mikali ya kidini.