Ugonjwa mpya wa ajabu wa kupumua uliogunduliwa nchini Argentina hadi sasa umeathiri watu 10, na tayari watatu kati yao wamefariki dunia.
Mamlaka za afya za Argentina zinajaribu kutafuta chanzo cha ugonjwa huo, ambao unasababisha matatizo ya homa ya mapafu (pneumonia), homa na maumivu ya tumbo.
Mgonjwa mpya wa kumi wa ugonjwa huo ameripotiwa kuwa mzee mwenye umri wa miaka 81 ambaye alitangazwa Ijumaa iliyopita na Wizara ya Afya ya Argentina katika jimbo la Tucumán. Wagonjwa wote 10 wamehusishwa na kliniki ya kibinafsi huko Tucumán.
Waziri wa Afya wa jimbo la Tucumán, Luis Medina Ruiz amesema Mzee huyo mwenye umri wa miaka 81, ambaye alikuwa mkazi wa Kituo cha Luz Medica, alilazwa katika hospitali hiyo akiwa katika hali mbaya.
Luis Medina amesema, wagonjwa wengine 9 ni wafanyikazi wa kliniki ambako ugonjwa huo umeripotiwa.
Wizara hiyo imesema watu watatu waliofariki dunia waliwahi kusumbuliwa na magonjwa mengine. Ruiz amesema kuwa miongoni mwa waliofariki dunia kwa ugonjwa huo wa ajabu ni mwanamke mwenye umri wa miaka 70 ambaye alifanyiwa upasuaji kwenye kliniki hiyo.