Nyerere alikuwa miongoni mwa viongozi wa kwanza wa Kiafrika kulitambua Shirika la Ukombozi wa Palestina (PLO) chini ya Yasser Arafat na, mwaka 1973, Dar es Salaam ikawa makao ya ubalozi wa kwanza wa PLO barani Afrika.
“Kizazi chetu kilikuwa kizazi cha mapambano ya utaifa kwa ajili ya uhuru wa nchi zetu … lakini hali ya Wapalestina ni tofauti sana na mbaya zaidi,” alisema Nyerere. “Wamenyang’anywa nchi yao wenyewe, ni taifa lisilo na ardhi yao wenyewe. Kwa hiyo wanastahili kuungwa mkono na Tanzania na dunia nzima.”
Ilikuwa ni katika muktadha huu ambapo mkutano wa Novemba huko Windhoek ulisisitiza uungaji mkono wake kwa watu wa Palestina katika mapambano yao ya kujitawala – angalau kwa sehemu kubwa.