Takwimu zinaonyesha kuwa, serikali ya Uingereza ni muuzaji wa pili mkubwa zaidi wa silaha kwa Saudi Arabia na mshirika katika uhalifu jinai zinazofanywa na muungano wa vita wa Saudia dhidi ya watu wa Yemen.
Uingereza ilishika nafasi ya sita duniani kwa mauzo ya silaha mwaka 2016-2020, ikiwa ni asilimia 3.3 ya mauzo yote ya silaha. Katika miaka hiyo, Uingereza imeuza silaha katika nchi 39 za dunia, na eneo la Asia Magharibi bado ni soko kuu la mauzo ya nje ya silaha za Uingereza. Saudi Arabia ndiyo mnunuzi mkubwa wa silaha za nchi hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti ya kila mwaka ya Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm, Marekani ilichangia asilimia 79 ya mauzo ya silaha za Saudi Arabia kati ya mwaka 2016 na 2020, ikifuatiwa na Uingereza yenye asilimia 9.3.
Wakati huo huo, Amnesty International imesema katika ripoti yake kwamba “nchi ambazo bado zinaupatia silaha muungano wa vita unaoongozwa na Saudi Arabia zitasajiliwa katika historia kama washirika katika uhalifu wa kivita nchini Yemen. Kuna ushahidi mkubwa kwamba mashambulizi ya kutowajibika ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia yamesababisha uharibifu mkubwa kwa raia wa Yemen.”
Kundi la wataalamu wa kikanda na kimataifa wa Umoja wa Mataifa pia linaamini kuwa mashambulizi hayo yanaendelea kupuuza sheria za kimataifa na maisha, utu na haki za watu wa Yemen. Katika kesi moja, mnamo Juni 2019, kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa na kampeni inayopiga vita biashara ya silaha ya serikali ya Uingereza, Mahakama ya Juu ya nchi hiyo iliamuru kusimamishwa na kupitia upya leseni ya uuzaji wa silaha kwa Saudi Arabia.
Melfu ya raia wa Yemen wameuawa na mamilioni ya wengine wamelazimika kukimbia makazi yao kuutokana na shambulizi ya Saudi na Washirika wake.