Vyombo vya habari vimeripoti kuwa serikali mpya ya Uingereza imelegeza kamba kuhusiana na mpango wa serikali ya waziri mkuu wa zamani Liz Truss wa kuhamishia ubalozi wa nchi hiyo katika mji wa Baitul Muqaddas (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu.
Tarehe 22 Septemba, wakati Liz Truss alipokutana na waziri mkuu wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel Yair Lapid mjini New York pembeni ya mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa aliahidi kuwa London itauhamishia ubalozi wake katika mji wa Baitul Muqaddas unaokaliwa kwa mabavu.
Ahadi hiyo aliyotoa Truss kwa Lapid ilipokelewa na kuungwa mkono na viongozi wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na ikapingwa na kulaaniwa vikali na waungaji mkono wa Palestina katika nchi mbalimbali
Msemaji wa Rishi Sonak ametangaza kuwa serikali ya waziri mkuu huyo mpya wa Uingereza haina mpango wa kuhamishia ubalozi wa nchi hiyo Quds tukufu inayokaliwa kwa mabavu.
Vyombo vya habari likiwemo shirika la habari la Ufaransa AFP vimeripoti kuwa serikali mpya ya Uingereza imeachana na mpango wa serikali iliyopita wa kuuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv na kuupeleka Quds, Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, msemaji wa Sonak amewaeleza waandishi wa habari: “hakuna mpango wa kuhamisha ubalozi wa Uingereza Israel kutoka Tel Aviv (kupeleka Quds inayokaliwa kwa mabavu)