Ujerumani yapiga marufuku shughuli za Kituo cha Kiislamu cha Hamburg

Serikali ya Ujerumani imechukua hatua ya kibaguzi ya kukifunga  Kituo cha Kiislamu cha Hamburg na mashirika tanzu nchini humo kutokana na kile ilichodai ni kueneza itikadi kali na idiolojia ya Kiislamu.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Nancy Faeser alisema katika taarifa yake siku ya Jumatano kwamba Kituo cha Kiislamu cha Hamburg (IZH) kitapigwa marufuku kwa “kufuata malengo ya Kiislamu yenye itikadi kali,” na kwamba ‘Msikiti wake wa Bluu’ uko chini ya ukaguzi mkali wa polisi.

Msikiti wa Imam Ali, ambao ni maarufu nchini humo kama Msikiti wa Bluu, ni mojawapo ya misikiti mikongwe zaidi ya Ujerumani na umekuwa ukiendeshwa na Kituo cha Kiislamu cha Hamburg.

Marufuku hiyo pia inalenga matawi ya Kituo cha Kiislamu cha Hamburg huko Frankfurt, Munich na Berlin.

Mwaka jana, Wizara ya Mambo ya Ndani iliishutumu Kituo cha Kiislamu cha Hamburg kwa “kwenda kinyume na utaratibu wa kikatiba,” na kuunga mkono harakati ya muqawama ya Hizbullah yenye makao yake Lebanon. Ikumbukwe kuwa Ujerumani iliitangaza Hizbullah kuwa eti shirika la “kigaidi” mnamo 2020.

Hizbullah ilikabiliana kijeshi na utawala haramu wa Israel ulipoivamia Lebanon mwaka 2000 na 2006, na kulazimisha jeshi hilo katili kurudi nyuma kwa madhila.

Katika ripoti ya kina mwaka jana, tume moja huru ya Ujerumani ilisema Waislamu nchini humo wanakabiliwa na ubaguzi wa rangi, chuki na vitendo vingine vingi vya ubaguzi kila siku.

Tume Huru ya Wataalamu iliyochunguza uadui dhidi ya Waislamu kwa miaka mitatu ilichapisha ripoti kuhusu ubaguzi wa rangi unaowakabili Waislamu wa Ujerumani, ikisema Waislamu nchini humo sio tu kwamba wanakabiliana na ubaguzi wa rangi bali pia wanalengwa na propaganda potofu za kila siku.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *