Ujumbe wa HAMAS waonana na Rais wa Syria mara ya kwanza baada ya miaka 10

Duru za Syria zimetangaza habari ya kukutana ujumbe mmoja wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na Rais Bashar al Assad wa nchi hiyo ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Televisheni ya al Mayadeen ilitangaza habari hiyo jana Jumatano na kuzinukuu duru hizo zikisema kuwa, ujuumbe wa Palestina wakiwemo wawakilishi wa HAMAS wameelekea nchini Syria na kuonana na Rais Bashar al Assad wa nchi hiyo.

Hii ni katika hali ambayo, juzi Jumanne, Msemaji wa HAMAS, Hazem Qassem alikuwa amesema kuwa, ujumbe wa Palestina ukiongozwa na Khalil al Hayah, mkuu wa ofisi ya Uhusiano wa Kiarabu na Kiislamu wa HAMAS utaelekea nchini Syria na kuonana na Rais Bashar al Assad.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, hiyo ni safari ya kwanza rasmi ya ujumbe wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS nchini Syria tangu mwaka 2012.

Tarehe 15 mwezi uliopita wa Septemba ilisema kuwa, ina nia ya kuimarisha uhusiano wake na serikali ya Syria katika pande zote.

Tarehe 21 Juni mwaka huu pia, duru moja ya Palestina ilitangaza kuwa, harakati ya HAMAS na serikali ya Syria zina nia ya kuanzisha tena uhusiano wao baada ya miaka 10. Uhusiano huo uliharibika baada ya kuanza mgogoro wa Syria.

Wakati huo Khalil al Hayah aliliambia gazeti la al Akhbar kwamba harakati ya HAMAS ina nia ya kweli ya kutatua mvutano wake na Syria.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *