Ujumbe wa kutambulishwa kwa Katibu Mkuu mpya wa Hizbullah nchini Lebanon

Mkakati wa kumtangaza Katibu Mkuu mpya wa Hizbullah ilikuwa hatua kubwa ya Hezbullah katika kuvuruga mpango uliobuniwa na utawala wa Kizayuni katika wiki za hivi karibuni.

Baadhi ya vyanzo vya usalama viliamini kuwa jina la Katibu Mkuu mpya wa Hezbollah linapaswa kuwekwa siri kwa ajili kuhifadhi usalama wake.

Hatahivyo Hizbullah haikufanya hivo (kuweka siri jina la katibu mkuu), bali hivi karibuni kundi hilo lilitangaza uteuzi wa  Sheikh Naim Qasim kama Katibu mkuu wa kundi hilo na kudhihirisha kua ana nafasi kubwa na uwezo wakushikilia nafasi hiyo kama mpokezi wa sehemu ya Sayid Nasrallah.

Ujumbe wa wazi wa Hizbullah ni kwamba haiko kimya katika masuala ya kijasusi na usalama.

Utawala wa Kizayuni ulitaka kupunguza uwepo wa kisiasa na kijamii wa viongozi wa Hizbullah kwa kuweka vikwazo vya usalama, lakini Hizbullah ilivuruga mlingano huu wa kijasusi kwa kumchagua na kumtambulisha hadharani Katibu Mkuu mpya.
Aidha Kuchaguliwa kwa Sheikh Naeem Qasim, kulizua fujo katika mfumo wa utawala wa Kizayuni.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *