Ujumbe wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS umewasili katika mji mkuu wa Russia, Moscow.
Ujumbe huo ambao unaongozwa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na Mkuu wa Ofisi ya harakati hiyo Ismail Hania unatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa nchi hiyo akiwemo Sergey Lavrov, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi hiyo.
Taher al-Nono, mshauri wa HAMAS katika masuala ya habari amesema kuwa, mbali na Ismail Hania, ujumbe huo unamjumuisha pia Moussa Abu Marzouk na Maher Salah na miongoni mwa mambo yanayotarajiwa kujadiliwa na uhusiano baina ya harakati hiyo na serikali ya Russia.
Kwa mujibu Taher al-Nono, mshauri wa HAMAS katika masuala ya habari ni kuwa, safari ya ujumbe wa harakati hiyo inafanyika kwa mwaliko wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia na kwamba, ujumbe huo unatarajiwa kubakia nchini humo kwa siku kadhaa.
Afisa huyo wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ameisifu misimamo ya Russiai kuhusiana na kadhia ya Palestina.
Safari hiyo inafanyika katika hali ambayo, utawala haramu wa Israel umeshadidisha hujuma na njama zake dhidi ya wananchi wa Palestina hasa baada ya mataifa kadhaa ya Kiarabu kuisaliti kadhia ya Palestina na kuamua kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel unaotenda jinai kila uchao dhidi ya wananchi wa Palestina.