Mohammed, Muqtada na Montazer Al-Kuwaiti ni ndugu watatu kutoka nchi ya Bahrain, wenye umri baina ya miaka 14 na 15, ambao walihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani na Al Khalifa mwaka 2021 kwa mashtaka ya uwongo pamoja na mateso na vitisho.
Wameshtakiwa kwa kushiriki katika maandamano, utengenezaji wa vifaa vinavyoweza kushika au kusababisha moto, kusababisha ghasia na uvamizi wa mali ya umma na ya kibinafsi.
Licha ya umri wao mdogo, wamekuwa wakikabiliwa na mateso ya kisaikolojia, matusi na vitisho.
Watatu hao walizuiwa kuonana na wazazi wao tangu walipokamatwa Juni 2021 hadi Februari 13, 2022, na baada ya hapo kufanyika mkutano uliokua chini ya uangalizi mkali kwa kamera.
Al-Khalifa amewazuiwa hata kuendelea na masomo, jambo ambalo linaashiria na kudhihirisha ukandamizaji wa wazi wa familia hiyo dhidi ya watu wa Bahrain.