Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika taasisi za kimataifa mjini Vienna, Austria amesema kuwa, kuanzia mwaka ujao Ulaya itaishi bila ya mafuta ya Russia kufuatia hatua yake ya kuainisha bei ya mafuta kutoka Russia.
Mikhail Ulyanov ametoa matamshi hayo akijibu hatua ya nchi za Magharibi na Umoja wa Ulaya ya kuianisha bei ya dola 60 kwa kila pipa la mafuta ya Russia na kuandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba: Moscow imesisitiza kuwa haitaziuzia mafuta nchi ambazo zinaunga mkono kuiainishia bei ya mafuta ya Russia.
Ulyanov ameudhihaki msmimamo wa nchi za Magharibi dhidi ya Moscow na kusema: Umoja wa Ulaya sasa unatazamiwa kuilaumu Russia kwamba inatumia suala la mafuta kama silaha dhidi ya Magharibi.
Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya Ijumaa iliyopita zilikubaliana kuainisha dola 60 kwa ajiilii ya kila pila la mafuta ghafi kutoka Russia yanayosafirishwa kupitia njia ya bahari.
Makubaliano hayo yataanza kutekelezwa kuanzia kesho Jumatatu.
Lengo la kuainisha bei kwa ajili ya mafuuta ghafi kutoka Russia ni kuipunguzia Moscow mapato yanayotokana na biashara ya bidhaa hiyo, huku vita vya Ukraine vikikaribia kuingia katika mwaka wake wa pili.
Baada ya Saudi Arabia, Russia ni nchi ya pili kwa kuuza kikubwa zaidi cha mafuta ghafi nje ya nchi na inasambaza takriban asilimia 10 ya mahitaji ya mafuta yasiyosafishwa duniani.