Katika hotuba yake hii leo, mkuu wa Umoja wa Afrika ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuzingatia ukandamizaji unaofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Ghaza.
Ghazali Osmani, Mkuu wa Umoja wa Afrika amesema kuhusiana na suala hilo: Jumuiya ya kimataifa haiwezi kufumbia macho ukandamizaji unaotokea Palestina.
Mkuu wa Umoja wa Afrika aliongeza: Tunawaomba viongozi wa Afrika kusaidia kumaliza mateso ya watu wa Gaza.
Kwa mujibu wa IRNA, siku 134 zimepita tangu kuanza kwa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza, huku juhudi za wapatanishi za kuupatia ufumbuzi mgogoro huo zikiendelea, vikosi vinavyoukalia kwa mabavu vinaendelea kufanya jinai katika ukanda huo wa kijiografia. Wanazua balaa na maafa mengine, safari hii katika mji wa “Rafah” ulioko kusini mwa Ukanda wa Gaza.
Wizara ya Afya ya Ghaza imetangaza leo kuwa, katika muda wa saa 24 zilizopita Wapalestina 83 waliuawa shahidi katika Ukanda wa Ghaza, na kwa njia hiyo idadi ya mashahidi tokea kuanza jinai za utawala huo ghasibu wa Kizayuni imefikia 28,858.
Wizara pia ilitangaza kuwa idadi ya waliojeruhiwa imefikia 68,677.