Umoja wa Mataifa: Udhalilishaji unaofanywa na serikali ya Sudan Kusini ni sawa na jinai za kivita

UN imesema kuwa viongozi na maafisa wa serikali ya Sudan Kusini wamekiuka haki za binadamu nchini humo; vitendo vilivyotajwa kuwa ni sawa na jinai za kivita. Ukiukaji huo wa haki za binadamu umewakumba pia watoto wa Sudan Kusini.

Nchi hiyo changa zaidi duniani imekuwa ikishuhudia mapigano na ukosefu wa amani tangu ipate uhuru mwaka 2011; ambapo Umoja wa Mataifa mwezi uliopita ulionya kuwa Sudan Kusini iko katika hatari ya kurejea katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kutokana na mizozo ya kikabila na mgogoro wa kisiasa unaotishia mwenendo wa amani unaolegalega.

Kamisheni ya Haki za Binadamu (OHCHR) huko Sudan Kusini jana iliwalisha ripoti ikieleza kuwa, ina sababu zote za msingi za kuamini kwamba, baadhi ya viongozi na maafisa wa serikali ya Juba wamehusika katika kukiuka haki za binadamu; vitendo ambavyo ni sawa na kutenda jinai za kivita. Ukiukaji huo wa haki za binadamu umetajwa kufanywa katika wilaya za Equatorial ya Kati na ile ya Magharibi, Kusini Magharibi mwa Sudan Kusini.

Yasmin Sooka Mwenyekiti wa Kamisheni ya Haki za Binadamu huko Sudan Kusini amesema kuwa, kamisheni hiyo imeandaa orodha ya watu 142 ambao wanatakiwa kuchunguzwa kwa uhalifu mbalimbali kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo na kimataifa.

Ripoti ya kamisheni hiyo imeutaja udhalilishaji mkubwa wa haki za binadamu kuanzia kubakwa pakubwa raia, wanawake kugeuzwa watumwa wa ngono hadi mauaji ya makusudi ya mamia ya watoto ikiwemo kisa cha kupigwa na polisi hadi kufa mtoto mchanga mbele ya mama yake.

Sooka amesema, mauaji  ya wenyewe kwa wenye, kuuliwa raia kwa umati, kuteswa, utekaji nyara, kuwekwa kizuizini raia, uporaji wa mali kuchomwa moto vijiji, wananchi kulazimishwa kuhama makazi yao, udhalilishaji wa kijinsia nk ni ishara ya wazi ya upinzani mkali wa kisiasa wa kuwania madaraka katika ngazi ya kitaifa huko Sudan.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *