Shirika la Afya Ulimwenguni lilitangaza Jumapili kwamba 70% ya sekta ya afya ya Sudan imeshindwa.
Tedros Adhanom, Katibu Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, ametembelea nchi hii katika safari ya siku mbili kuangalia hali ya Sudan.
Katika mkutano na waandishi wa habari katika eneo la Bandar Sudan, alisema kuwa tangu mwezi Aprili 2023, zaidi ya watu 20,000 wamekufa kutokana na migogoro ya nchi hii.
Aidha Adhanom ameongeza kuwa tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan, watu milioni 10 walikuwa wakimbizi wa ndani na wengine milioni 2 walilazimika kuwa wakimbizi katika nchi jirani.
“Hatua za Dharura zimefanywa ili kupunguza mzozo na kukabiliana na mateso yanayotokana na (vita) japo juhudi hizo hazijatosha kupunguza tatizo lililopo,” katibu mkuu wa WHO aliongeza.
Aliendelea kusema kuwa karibu nusu ya wakazi milioni 25 wa nchi hiyo wanahitaji msaada na asilimia 70 ya sekta ya afya ya Sudan iliyopo nje ya utaratibu.
Umoja wa Mataifa umeuita mzozo wa Sudan kama “moja ya maafa mabaya zaidi ya kibinadamu katika historia ya hivi karibuni.”